MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kelele zinazoendelea dhidi yake ni dalili za mafanikio katika vita dhidi ya dawa za kulevya.
Makonda ameyasema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi katika tamasha la Twendezetu Kigamboni lililofanyika katika wilaya.
Amesema, mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni ya kufa au kupona.
“Mfahamu kuwa tunapambana kati ya mauti na uzima, kelele, mwangwi vinavyoendelea sasa ni dalili njema kwamba tunaendelea kunyooka,” amesema Makonda.
Makonda alisema Dar es Salaam ya sasa anaifananisha na chuma kilichopinda na sasa kiko katika hatua ya kunyooka hivyo lazima zitokee kelele nyingi kama ambavyo zinaendelea sasa.
“Huwezi kufanya kazi ya kunyoosha chuma bila kusikia mwangi, kelele na maumivu kwa sababu kazi ya kukomboa vijana dhidi ya dawa za kulevya si rahisi,” amesema Makonda.
Amesema katika kipindi hicho ambacho amekiita kuwa ni cha kulinyoosha Jiji la Dar es Salaam ni lazima kelele zisikike, uonekane moto unaoacha maumivu makali na baada ya hapo ije picha ya chuma kilichonyooka ambayo ndio picha ya Jiji la Dar es Salaam itakayokuwa imenyooka.
Amesema kelele hizo zitapita na mwisho lazima kufika ng’ambo ya pili pasipo na dawa za kulevya, kwenye taifa lililojengwa na uchumi imara.
Amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa ambapo alisema hivi sasa katika Jiji la Dar es Salaam dawa hizo zimepungua.
“Nitoe pongezi kwa Jeshi la Polisi dawa za kulevya zimepungua sasa Dar es Salaam na pia niwapongeze pia vijana ambao wanaendelea kutoa taarifa,” alisema Makonda.
Aliwaasa wananchi kushirikiana na Rais John Magufuli ambaye anafanya jitihada kuijenga Tanzania ya kesho iliyo bora. Kuhusu Kigamboni alisema anatarajia kuiona Kigamboni ikiwa mji wa mfano ambao haujaharibiwa na matendo yasiyofaa ikiwa ni pamoja na uhalifu na vijana walioharibika kutokana na matumizi ya dawa za kulevya badala yake kuwe na vijana wachapakazi.
“Watu watakapokuja Kigamboni wakute ni mji msafi, salama, uliopangika unaofaa kupumzika… mji ulio salama usio na uhalifu,” amesema Makonda.
Amewataka wakazi wa wilaya hiyo kushirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa na viongozi wake katika kutimiza ndoto hiyo ya kuifanya Kigamboni tulivu na salama.
Amewaasa wazazi kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya watoto wao kuhakikisha hawajiingizi katika matumizi ya dawa za kulevya na pia vijana kuchungana wao wenyewe.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Mgandilwa alisema lengo la tamasha hilo ni kuzitambulisha fursa zilizopo katika wilaya hiyo, kuwakutanisha vijana kupiga vita dawa za kulevya na pia kuiunga mkono serikali katika kufanya mazoezi.
Tamasha hilolilihudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Faustine Ndungulile Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Rahel Mhando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.
Arrogant. Sihui nani abampavhii arrogance kujiona juu ya sheria kama Mungu.kamavsheria ya nchi ni kuhakiki vyeti dare him.nanivyupo nyuma ya huyuvkijana mwenye kichwa kupita Mungu. Ni Kiwete au Pombe. Kuna sheria za nchi. Na si mtu si Raisi.
ReplyDeleteKiukweli umejitahidi sana kupambana na madawa ya kulevya hongera. Ila huna budi kujisafisha kW hili zoezi lakitaifa LA vyeti feki na serikali haina haja yakuendelea kupanbana na wenye vyeti feki kama TU VIONGOZI WAKUBWABWA KITAIFA WANAHUSISHWA MAANA WANABIDI KUWA NDIO MFANO NA SIKUWAUMIZA WANANCHI WA HALI YA CHINI. SHERIA NI MSEMENO HUKATA HUKU NA KULE so mweshimiwa makonda unabidi uwajibike kwa hili ila mazoezi mengine yaweze kuendelea vizuri.
ReplyDeletetoa vyako kwanza harafu tutamwambia Makonda naye atoe na gwajima atoe na vya kwake
Deletewatanzania pambafu kabisa mnakubali kufitinishwa na kiongozi wenu kwa fitina ya Gwajima je hivyo vyeti feki anavyovisema Gwajima mmeviona na kuthibisha ni kweli feki kazi kulumbana na maneno mbofumbofu bila mpango mtoleeni povu Gwajima avianike hadharani vyeti feki vya Mkuu wa mkoa Mr. Makonda ndo mjue kumng'ania Makonda sio kila muambialo ni kutoleana mapovu sasa hata watumiaji wa madawa nao wanahoji eti Makonda awaridhishe kwa kuonyesha vyeti vyake halali
ReplyDeleteBIG UP BROTHER. MUNGU ATAKUSIMAMIA MAANA UNAPIGANIA KUOKOA VIJANA AMBAO NI NGUVU YATAIFA. UKIONA ANAYETAPATAPA HILO NI JIPU NA NDIO MHUSIKA WA HAYO MADAWA. KAMA UKO SMART HUTUMII WALA HUUZI KWANINI USISUPPORT KAZI NGUMU ANAYOIFANYA MH. MAKONDA?
ReplyDelete