Makosa ya Kitaalamu Aliyoyafanya Askari Aliyemuonyesha Bastola Nape..!!!


Tukio la kuzuiwa Mkutano wa Mh Nape kuzungumza na wanahabari ni jambo mtambuka, mimi leo nataka nilichambue tukio la askari kumtishia bunduki bwana Nape Nnauye. Naliangalia katika mtazamo wa kitaalamu zaidi.

Kwanza tujifunze mambo machache,
Polisi nini? Hili watu wamekuwa wakilichanganya, Kuwasaidia maana ya neno POLICE ni People's Oorder, Law, lnvestigation and Criminal Enforcements kwamjibu wa Wagiriki, lakini Wazungu wanasema ni Law enforcement and criminal investigation..not vice Verser. Kisha tujifunze utendaji kazi wa huyu mtu aitwaye polisi upoje hapa Tanzania na duniani kote, kwakuwa sheria ni moja japo zinaweza kutofautia kidogo tu kimaumbile na kiutekelezaji lakini msingi wake ni mmoja.

Criminal investigation procedure kupitia criminal investigation Act inamruhusu askari kutumia nguvu pale tu mtuhumiwa anapoonesha ubishi wa kutotii.

Pia sheria hiyohiyo inamtaka, hii ni lazima sio ombi, askari kujitambulisha ikiwa ni Pamoja na kuonesha kitambulisho kabla "hajaanza" utekelezaji wa majukumu yake.

Kwa dhana na uhalisia wa video hii ninayoitumia kama msingi wa uchambuzi, Mh Nape alikuwa sahihi kumuuliza yeye ni nani na akaomba kitambulisho. Kwa hatua hiyo tu, yule askari ana makosa hata kama ni askari uliyevaa sare au umevaa kiraia kama huyu, ukitaka kumkamata mtu lazima ujitambulishe wewe nani na unatokea kituo gani kisha ufanye yako kwa raia sio kwa kwa utaratibu ule hata kwa mazingira gani, Nape pia ana haki yakujua huyo polisi ni nani.

Suala la kutoa silaha lina mambo mengi ya kitaalamu, Kisheria askari popote ulipo katika misheni yoyote unatakiwa kuwa armed muda wote, lakini kuwa armed si kumpoint mtu gun ambaye ni unarmed wala hajaonesha dalili ya madhara kwako. Hili ni kosa kubwa kwa askari huyu.

Polisi yule anaweza kuwa na utetezi wenye hoja na usipokuwa makini unakubaliana naye kwamba aliona Nape yupo peke yake ndio lakini alikuwa amezungukwa na watu anaoamini ni wafuasi wake. Katika mazingira kama yale ambayo watu wengi wamejaa ambao kwa tafsiri ya kawaida ni watu wanaomuunga mkono nape, unategemea silaha itoke baada ya vurugu kuanza? Hii ni hoja nzito na inamruhusu askari kutoa silaha, lakini hoja hiyo inakufa kwenye kitendo cha kumuelekeza silaha mtu aliyesimama na hana silaha yoyote,

Askari huyu anaweza kujitetea tena kwamba alipomuona mtuhumiwa huyu kasimama alikuwa ameweka mikono mfukoni mwa suruali yake hali iliyomfanya yeye askari afikiri huyu mtu ana silaha,hivyo akamuwahi kwakunyooshea silaha.

Lakini utetezi huu unafutwa na kitendo cha yeye awali kwenda moja kwa moja kwa mtuhumiwa na kumshika na kumsukuma arudi kwenye gari, sauti ya video inasikika mtuhumiwa akimtaka mtu huyu anayedhaniwa ni askari ajitambulishe kwa kuonyesha kitambulisho jambo ambalo lilikuwa rahisi tu lakini ghafla akachomoa silaha na kumnyooshea mtuhumiwa.

Lakini nikitumia video hii namuona askari huyu anatumia silaha kizembe sana huyo angekutana na wenye mafunzo angekuwa chini silaha ingenyang'anywa,.

Kwaasili ukimtazama anaonekana akiihamisha silaha mkono wa kulia baada ya kuitoa kwa mkono wa kushoto,hii inamaana anatumia mkono wa kulia, lakini silaha aliweke kiunoni upande wa kushoto, hali inayomfanya achelewe kuichomoa kiunoni, silaha inatolewa zaidi ya sekunde 60 mpaka anapigwa picha nyingi, tazama hiyo picha Nape angekuwa mtaalamu wa mapigano ya kujihami kijasusi alikuwa anaweza kupiga teke au kifuti na kushika mkono wenye silaha na kumpora.

Kosa la pili ni la polisi waliomzunguka huyu aliyetoa silaha mpaka wakaacha raia Maulidi Kitenge kumvaa yule askari.

Tena Maulid Kitenge japo huenda hajui sheria lakini kafanya kosa kubwa sana kuwaingia wakati wakitimiza kazi zao. Kwa askari makini huyu Kitenge tungeimba iyena iyena leo. Ni kwa kosa la baadhi ya Wanausalama kuwa Wabaridi kumwacha Maulid amsukume Afisa active katika situations ile. Ukweli Maulid kawaponza askari walio Dormant hadi akaingilia mission kiasi cha kuhatarisha Usalama wa mwenzao ambae Silaha yake tayari alikwisha weka kwenye chamber

Kwa minajiri hii, Askari waliokuaa kwenye opaesheni hii wanatakiwa kuwajibishwa kwa ukiukwaji kwa sheria kanuni na taratibu za kazi ya uaskari wao,

Lakini askari aliyetishia kwa silaha atakiwa kuadhibiwa kwa uzembe, suala lake ninadhani huwezi kulipeleka kwenye mahakama ya kiraia labda ya kijeshi, kwa mtazamo wangu, yale ni makosa katika oparesheni za kiusalama ambapo anaweza kushitakiwa katika mahakama ya kijeshi. Msingi wa kesi ya kiraia unaweza kuita ni kvamiwa na mtu mwenye silaha anayedhaniwa ni jambazi. Wataalamu wa sheria za kiraia kina Tundu Lissu, Peter Kibatala, John Mallya, Ben Alex Ishabakaki, Jebra Kambole Sr. Na wengine mnaweza kulifafanua vizuri hili...

Na Yericko Nyerere

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad