Makubwa Haya..Mkuu wa Wilaya Akataza Watu Kula Kitimoto..Kisa Hiki Hapaaa..!!!


Walaji wa nyama ya nguruwe ‘kitimoto’ wilayani Kalambo mkoani Rukwa watakikosa kitoweo hicho kwa muda usiojulikana baada ya Serikali kupiga marufuku watu kula nyama hiyo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya nguruwe 150 kufa kwa ugonjwa wa mafua wa African Swine Fever na kuwaacha wengine wakiwa hoi.

 Mkuu wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Julieth Binyura alisema ugonjwa huo ulijitokeza miezi mitatu  iliyopita kwenye Kitongoji cha Masazi  na kusambaa  katika kata za Legezamwendo  na Mambwe Nkoswe.

Ofisa Mifugo wa Wilaya ya Kalambo, Wilbroad Kansapa  alisema nguruwe wote wanaozagaa mitaani watakamatwa na mizoga yote ifukiwe.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. "Makubwa haya"uandishi wa kishabikishabiki.

    ReplyDelete
  2. yani hii habari umeiandika kidaku kweli
    we mwandishi sijui wa wapy?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad