NIMEKUKUMBUKA leo mama wa muigizaji Wema Isaac Sepetu. Habari za hapo Sinza-Mori, familia yako haijambo? Vipi mnaendeleaje? Najua utashangaa kwa nini leo nimekuandikia barua lakini usishtuke, huu ni utaratibu wangu wa kila wiki.
Huwa nawaandikia watu mbalimbali mashuhuri kama wewe mama. Eeeh! Mwanao amekufanya na wewe usikauke kwenye vyombo vya habari. Hongera yako. Labda tu nikuibie siri kidogo mama, barua hii ni tofauti na zile nyingine ambazo mara nyingi huwa zinasomwa na watu wawili; muandikaji na muandikiwa.
Barua hii inasomwa na mamilioni ya Watanzania ambao watapata fursa ya kujipatia nakala tu ya gazeti hili kwa shilingi mia tano.
Hilo si dhumuni la kukuandikia barua hii. Ngoja nienda moja kwa moja katika hoja. Mama nimekuandikia kwa lengo moja tu, kukuambia kwamba hukupaswa kumfanyia vile muigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ katika sakata lako na mwanao, hata kama ulikuwa una lengo la kumtumia kama ‘silaha’ kwenye vita unayoiendesha.
Mosi, kwa heshima uliyonayo kitendo tu cha kumrekodi (naamini upande wa simu yako ndiyo ulirekodi, yaweza pia kuwa vinginevyo), kilikuwa si cha kiungwana. Kitendo kile pengine kingefanywa na vijana kwa vijana, kidogo kingeeleweka lakini si wewe kama mzazi.
Pili, kama alivyosema Steve, kwa wazo lako la kurekodi limesababisha pia wewe usikike ukifanya masihara ambayo kama ni kweli umehusika kuyasambaza, ukitafakari vizuri utaona jinsi gani yanakurudia wewe mwenyewe.
Yanakudhalilisha maana umesikika ukizungumza mambo yasiyopendeza kutamkwa na mtu mzima mbele ya hadhara. Kitendo cha wewe kuaminika umemrekodi Steve, kimeleta matokeo ya wewe kuvujisha utani wa kijinga usiopendeza kwa mama na mwanaye.
Steve amesikika akikutania kwamba anataka mzae mtoto, utani mbaya ambao kwa namna moja au nyingine, haupendezi kusikika na mamilioni ya Watanzania. Kwa anayewaza vizuri, hawezi kumrekodi mtu katika mambo ya siri kama yale na kwa namna yoyote ile kuyarusha mitandaoni.
Niliposikiliza ile sauti, kwangu niliona ni kama matusi. Mama yangu, jambo lile lingefanywa na vijana wenzake Wema, lingekuwa na picha yenye ahueni lakini wewe kusikika unatoa lugha chafu kwa kijana kama utani, ni aibu.
Jamii nzima itapata tabu sana kukuamini hata kama ulikuwa na lengo jema katika jambo hilo au umevurugwa kiasi gani. Kama mama, hata kama umekosewa, waswahili wanasema huwezi kumfukuza chizi akiwa mtupu na wewe ukiwa mtupu.
Utajistahi kwanza ndipo umkimbize. Kwa namna yoyote, heshima yako inapaswa kubaki palepale. Kama Steve alivyosema, hakutegemea ungeweza kumrekodi kwani anakuheshimu kama mzazi wake. Steve alisema alizungumza na wewe kirafiki kama mama na mwanaye.
Alizungumza na wewe akiamini huwezi kumsaliti au kumfanyia vitendo vitakavyomhatarishia maisha yake ya baadaye kama ulivyofanya. Pamoja na hayo yote, kama vile mlivyokuwa mnaitaka haki na mwanao, hamkupaswa kuidai kwa kuvunja haki. Maana kwa
mujibu wa sheria ya makosa ya mtandao ni dhahiri itakugusa kwa namna moja au nyingine. Yale ni mazungumzo binafsi, yametokaje kwenye mitandao ya kijamii? Mwisho, nikushauri, wewe ni mzazi kuna mambo ambayo unapaswa kuyazungumza mbele ya jamii mengine weka akiba. Si vyema ukawa unatengeneza picha kwamba kila ukionekana, utamwaga povu kama ulivyosema siku ile kwenye mkutano wa waandishi wa habari.
Naamini mama utakuwa umenielewa. Nimezungumza kiungwana, naomba nawe uwe muungwana katika kila hatua unayopiga kwenye safari yenu na kila unalolifanya, ni vyema kufikiri mara mbilimbili na kujua hatima ya jambo unaloliamua.
vizuri sana mwandishi>asiye funzwa na mamae hufunzwa na ulimwengu..ndo huyo mama..yeye mwenyewe alikuwa anaona anajiosha kumbe anajichafua tena kwa kutumia kinyesi..daddek..
ReplyDeleteJamii imesha kudharau kusiko na mfano/down down down..cheap easy like that..
ReplyDeleteNilichokiona hapa ni kweli kuna au kulikuwa na mahusiano ya kimapenzi kati ya Steve na mama Wema,na haishangazi kwa dunia ya leo wa mama kutoka na serengeti boys,Na ndio maana wakati steve anamuambia wazae mama wema alikuwa anaipotezea kinamna fulani,Utani gani huo kwa mama na mwana?
ReplyDelete