Mambo 6 Yanayomponza Paul Makonda...!!!


Bado Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (36) anaendelea kutajwa kwenye vinywa vya Watanzania wengi kufuatia madai ya kutumia vyeti ambavyo vinasemekana si vya kwake, lakini Amani sasa limebaini mambo 6 yanayomponza bosi huyo.

Kwa takriban wiki ya tatu sasa, jina la Makonda limekuwa likiandikwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwa ishu hiyo ya vyeti ambapo, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar, Joseph Gwajima ndiye aliyeibua madai hayo mazito kiasi cha kuifanya jamii kuyavalia njuga madai hayo.

ILIKUWA KWENYE IBADA YA JUMAPILI

Gwajima aliibua sintofahamu ya vyeti hivyo, Jumapili ya Februari 26, mwaka huu, kwenye mahubiri ya ibada ya kanisani kwake, Ubungo ambapo alisema kuwa, Makonda anatumia cheti cha kidato cha nne cha mtu anayeitwa Paul Christian Muyenge wakati yeye alianza darasa la kwanza mwaka 1988, akitumia jina la Daudi Albert Bashite.

Akihubiri huku waumini wake wakimsikiliza kwa umakini mkubwa, Mchungaji Gwajima alisema kuwa, mwaka 2001, Makonda alitumia cheti cha mwanafunzi huyo chenye divisheni 3 ya ponti 25 ili aweze kujiunga na Chuo cha Uvuvi Nyegezi (NFTI) na ndiyo akaendelea hivyohivyo mpaka kufi ka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi na baadaye kuingia kwenye siasa na leo hii ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

MAKONDA HAPENDWI?

Tangu kuingia kwenye siasa, Makonda amekuwa akikumbwa na ‘bahati mbaya’ ya kuwa na damu ya kunguni kiasi kwamba, kwa tafsiri ya kawaida ni rahisi kusema kuwa, baadhi ya watu hawampendi lakini ni kutokana na utendandaji wake uliotukuka.

AMANI LABAINI MAMBO 6 YANAYOMPONZA

Amani liliweza kuzungumza na baadhi ya watu kuhusu utendaji kazi wa Makonda ambapo wengi walitoa maoni yao kwamba, yapo mambo yaliyosababisha mheshimiwa huyo kuingia kwenye kuonekana na watu ‘ana damu ya kunguni’ na ndiyo yanayomponza.

JAMBO LA KWANZA, WAKATI WA BUNGE LA KATIBA

Mwaka 2014, chini ya utawala wa Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’ Tanzania iliingia kwenye mchakato wa Katiba Inayopendekezwa ambayo Jaji Joseph Warioba alikuwa mwenyekiti wa kutafuta maoni mitaani. Baada ya maoni kukamilika, kulikuwa na mijadala mbalimbali ikiendelea, ikiwemo kuundwa kwa Bunge la Katiba ambapo, Makonda alikuwa mmoja wa wajumbe walioteuliwa na JK. Katika mjadala mmoja uliofanyika kwenye Jengo la Ubungo Plaza jijini hapa na Jaji Warioba akiwa mshiriki mkuu, kulitokea vurugu kubwa kiasi kwamba, mzee Warioba alidaiwa kupigwa.

Mengi yalisemwa, baadhi ya watu walidiriki kutamka kwamba, miongoni mwa watu waliompiga mzee Warioba ni Makonda. Ilibidi Makonda atumie nguvu kubwa kukanusha kwamba, yeye siye aliyempiga mzee Warioba bali aliingilia kati kuamua na kumuweka sawa mzee huyo aliyewahi kuwa waziri mkuu mwaka 1990.

Hata hivyo, licha ya utetezi wake, Warioba mwenyewe alitoa tamko kwamba hakupigwa na Makonda, lakini watu walishindwa kumwelewa mzee huyo na kuendelea na madai kwamba ni Makonda tu. Kuanzia hapo, jamii ilianza kumuona Makonda kama si mjamii kwa tukio la kusema alimpiga mzee Warioba na kukatokea mgawanyiko wa watu, waliomshabikia na waliokataa kumshabikia ambao idadi yao kama iliuelemea mzani.

MKUU WA WILAYA

Nyota ya Makonda licha ya madai ya kumpa kichapo mzee Warioba, ilizidi kung’ara, kufumba na kufumbua JK akampa ukuu  wa wilaya ya Kinondoni ambapo kwa hakika, alijitokeza mstari wa mbele kutatua migogoro ya ardhi na kuonekana kwenye vyombo vya habari kila kukicha kwamba, anatetea wanyonge. Wapo waliomkubali kwa kazi hiyo, wengine waliendelea kuwa na msimamo uleule kwamba hawamkubali.

JAMBO LA PILI, NAULI ZA WALIMU DAR

Bado akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Makonda aliwahi kutoa ofa ya walimu wa Jiji la Dar kupanda bure daladala. Lakini siku ya kwanza ya zoezi hilo hakuna mwalimu aliyekubali kulipiwa nauli wakidai kuwa, wanaweza kujilipia wenyewe. Nyuma ya zeozi hilo ilisemekana kuwa, walimu waliwahi kukerwa na matamshi ya Makonda siku za nyuma kuhusu walimu na madaraja yao ya kazi.

Kwa hiyo walimu nao wakamuona Makonda ni ‘adui’ yao. Mwaka 2015, mwaka mmoja tu baada ya Bunge la Katiba, akaingia madarakani Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ huku Makonda akiendelea kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, lakini kabla ya kupepesa macho, JPM akamteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ‘RC’. Hapo ndipo yakaongezeka mambo juu ya mambo.

JAMBO LA TATU, APIGA VITA SHISHA, MASHOGA NA MACHANGU

Makonda aliingia kwenye kiti cha u-RC akiwa na munkari wa kufanya kazi, alihakikisha jiji linakuwa safi  kwa wakazi wake kufuata maadili na kuachana na maisha ya mkato. Kwa hiyo alipiga vita matumizi ya kilevi aina ya shisha, akatangaza vita na wanaume tata ‘mashoga’ lakini pia akawaambia wanawake wanaojiuza ‘machangudoa’ kwamba, waachane na biashara hiyo mara moja.

Makundi ya watu yakaibuka na kudai; ‘Makonda anajifanya ni mchapakazi sana ili rais ampende’. Kwa hiyo akaongeza sababu nyingine ya kuwa na ‘maadui’ kwani wavuta shisha walikasirishwa kwa kuondolewa kwa starehe yao hiyo achilia mbali mashoga na machangu ambao walimuona anawakomalia hivyo kuwahatarishia njia zao haramu za kupata kipato.

JAMBO LA NNE, ZOEZI LA DAR ES SALAAM MPYA

Siyo siri wala hakuna sababu ya kupepesa macho, miongoni mwa mambo ambayo, yalimwongezea ‘maadui’ Makonda ni oparesheni ya Dar Mpya ambayo aliifanya kwa nia  njema ya kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi wa mkoa wake huo wenye watu karibu milioni 6. Zoezi hilo lilifanyika kwa siku karibia saba ambapo Makonda na wasaidizi wake walikuwa wakifanya mikutano ya hadhara kila siku katika maeneo mbalimbali na kusikiliza kero.

Katika kusikiliza kero hizo  baadhi ya watu, hasa viongozi wa serikali za mitaa na wengine, walijikuta wakikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya kutuhumiwa hadharani.

Mbaya zaidi ili watuhumiwa hao wakamatwe, Makonda alikuwa akiamuru kwa sauti na kuwanyooshea vidole mkutanoni huku kituo kimoja cha runinga jijini Dar kikirusha mubashara matukio hayo hivyo wengi kudai ni udhalilishaji.

Baada ya mikutano ya Dar es Salaam Mpya kumalizika, baadhi ya watu walikuwa mahabusu, wengine mahakamani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofi si au pesa, lakini huku Makonda mwenyewe akiwa ameongeza idadi ya ‘maadui’.

JAMBO LA TANO, MATAMSHI YAKE

Katika mikutano hiyo, watu wengi walikuwa wakilalamikia kitendo cha Makonda kuwasemea maneno makali viongozi waliokuwa wanatuhumiwa kwamba, hakuwa anajali umri wao na hivyo kusema lolote lile.

“Kwenye ile mikutano ya Dar Mpya hakuna jambo lilikuwa likiniumiza kama matamshi yake Makonda. Unajua wengine walikuwa sawa na wazazi wake, lakini yeye akawa hachagui maneno ya kusema. Unajua ulimi siku zote bwana ndiyo wenye kuleta tatizo.

“Ni vyema kiongozi akawa anaingiza maneno yake kwenye kipimo kwanza kabla ya kutoa sauti. Kipimo cha kazi yake ni kuchuja, kwamba hili niliseme, hili hapana,” alisema Hussein Mohamed, mkazi wa  Buguruni na kuongeza:

“Unajua inawezekana kabisa, kule kupendwa sana na rais ndiyo kumempa ‘kichwa’ cha kutoa kauli kali za namna ile.”

JAMBO LA SITA, MADAWA YA KULEVYA Licha ya kuacha ‘majeruhi’ kibao  kwenye zoezi la Dar Mpya, bado Makonda kama kawaida yake, hakuacha kujipa ujasiri na kufanya kazi ya kutumikia wananchi na kupinga mambo yaliyo kinyume na uadilifu, hivyo Februari 2, mwaka huu, Makonda kwa mara ya kwanza na akiwa mkuu wa mkoa wa kwanza nchini, alijitokeza hadharani na kutaja majina kadhaa ya watu aliodai wanajihusisha na madawa ya kulevya.

Katika majina hayo, yalikuwepo ya watu maarufu, akiwemo Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na askari polisi 12. Makonda aliwataka watu hao kufi ka kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar kwa mahojiano ambapo walitii.

Baada ya sakata hilo, Februari 8, mwaka huu, Makonda akaibuka na listi kama siyo orodha ya watu wengine 65 akiwataja majina na kuwataka wafi ke kwenye kituo hichohicho cha polisi kwa ajili ya mahojiano. Miongoni mwa watu hao, walikuwemo wenye majina makubwa nchini kama vile, mfanyabiashara Yusuf Manji, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni (Chama Cha Mapinduzi), Idd Azzan na Gwajima ambaye ndiye aliyeibua hoja ya vyeti.

‘MAADUI’ WAONGEZEKA’ Kitendo cha Makonda kutaja majina ya wadaiwa kujihusisha na madawa ya kulevya hadharani kiliibua hoja nyingine, wengi walijitokeza wakipinga kwamba, hakuwa sahihi kwa sababu watu hao ni watuhumiwa tu.

Hoja hiyo ilipaa juu zaidi hadi kufi kia kushika mjadala mkubwa nchini kwamba ni sahihi au siyo sahihi? Miongoni mwa watu waliokereka na kutajwa ni Gwajima.

Yeye alisema kuwa, Makonda alimtendea sivyo hivyo akatangaza vita naye. Katika vita hiyo, ndipo Gwajima naye akadai amechimba na kuchimbua na kubaini kuwa, Makonda alitumia vyeti vya mtu mwingine kuingia chuo baada ya yeye kufeli hivyo akamtaka Rais Magufuli  kumwajibisha.

NIA YAKE NI NJEMA

Katika mtazamo wa kawaida, katika yote aliyoyafanya au kuyasimamia Makonda yana njia njema kwa jamii. Nani asiyejua madawa ya kulevya yanavyoathiri jamii? Nani asiyejua shisha inavyoharibu vijana? Nani asiyejua ukahaba unavyoweza kuleta magonjwa? Lakini pengine uwasilishaji wake ndiyo umekuwa ukisumbua wengi.

NDIYO YAMEMPONZA

Makonda leo hii kama asingetaja hadharani majina ya watu wa unga, kama asingejitolea kuwapiga vita machangu na mashoga, kama asingewakera walimu kwa nauli, kama asingefanya mikutano ya Dar Mpya ina maana angekuwa ni mkuu wa mkoa aliyepoa na kuonekana mwema machoni kwa watu. Kumbukumbu ziko hivyo, wale wanaojitoa mhanga kusimama mbele za watu na kupambana kwa dhati kukosoa matatizo hukumbwa na vita kubwa kutoka kwa watu wenye

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad