Mbowe: Madaktari Msiende Kenya, Rais Anacheza na Maisha Yenu, Kenya Sio Salama kwa Sasa..!!


CHADEMA tunasema hivi, Rais Magufuli acha mchezo wa kucheza na maisha ya madaktari wetu, katika mazingira ya kawaida, ingekuwa wanakwenda Kenya wakati kuna hali ya utulivu, kuna hali ya uhakika wa Usalama Kenya tungeruhusu vijana wetu wakafanye kazi kwa sababu hata Wakenya ni ndugu zetu, lakini katika mazingira ambayo kuna mgomo Kenya, kuna kutoelewana kati ya Serikali ya Kenya na madaktari wao, sisi ndio tuwe kimbelembele cha kuwatoa watoto wetu kwenda kutibu Kenya wakati Wakenya wenyewe hawawataki ni kuweka maisha ya Watanzania wenzetu , wataalam wetu katika risk, sisi Kama Chama Kikuu cha Upinzani tunapinga, na naomba Mkutano huu Mkuu wa Kanda ya Pwani utoe tamko la kupinga madaktari wetu kwenda nchini Kenya.

Magufuli na Serikali yake wawape ajira vijana wetu vituo vya afya havina madaktari, Sera yetu ya Taifa inasema vituo vyetu vya afya lazima vihudumiwe na madaktari lakini mpaka leo hakuna madaktari kwenye vituo vya afya kwa sababu Serikali imeshindwa kuajiri.

Kwa hiyo wapo vijana wengi kwa muda wa miaka miwili hawajaajiriwa lakini suluhu sio kuwakimbizia nchi za jirani ambazo zina migogoro na wataalam wao, suluhu ni Serikali yetu itafute fedha iwaajiri vijana hawa, mama zetu, wazee wetu, vijana wetu wanawahaitaji madaktari hawa wawatibu katika vituo vyetu vya afya katika zahanati zetu katika hospitali zetu, Kwa hiyo naomba Mkutano Mkuu Maalum wa Kanda Pwani, naomba mnikubalie Kama Mwenyekiti wa Chama kupitia Mkutano huu tutoe tamko hili rasmi la kupinga madaktari wetu kwenda nchini Kenya.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ww mbowe unaposemaga waandamane au wasiondoke vituoni wakae wlinde kura huwa huoni kuwa ni salama kwa vijana wa Tanzania eh ila kwa kwenda Kenya ndo siyo salama duh nyie wapinzani ni nouma aisee

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad