MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema Rais Dk. John Magufuli atakuwa kiongozi wa kwanza nchini kuvunja rekodi ya kutawala kwa kipindi cha miaka mitano badala ya 10 kama walivyofanya watangulizi wake.
Mbowe aliyasema hayo jana wakati akizindua tawi la wakereketwa wa chama hicho lililopo eneo la Mpakani, Kata ya Kwakifua, Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Katika hoja hiyo, Mbowe alisema Rais Magufuli ataongoza kwa muhula mmoja kwa kuwa utawala wake hauthamini utu wa binadamu, na ikiwa vinginevyo, yuko tayari kuachana na siasa. “Watu wa Tanga mmechelewa sana kuiondoa CCM madarakani, tulifanya makosa kumchagua Rais wa Awamu ya Tano, matokeo yake wote tunaisoma namba. Tunaanza maandalizi mapema, maana huyu rais atatawala miaka mitano na akiendelea naacha siasa,” alisema Mbowe. #Mtanzania .
JE NI KWELI ANAYOSEMA MBOWE??? TUPIA COMMENT YAKO HAPA
Kushinda au kutoshinda itategemeana watamsimamisha nani. Kwanamba kweri watu wanasema namba sio Siri
ReplyDeletemawazo ya Kichovu
ReplyDeleteHivi wewe Mbowe ni mwenye hati miliki wa chadema ondoka kwanza wewe achia uenyekiti wa kidikiteta umeng'ang'ania miaka nenda rudi hadi kina magufuli wanakukuta hujang'atuka unataka walioshika madaraka jana ndio waachie madaraka eti muhula mmoja jamani wabongo tukoje bado tunaishi ktk maisha ya dhana kuwamilikisha demokrasia yetu kina mbowe eti ndo watetezi wa demokrasi
ReplyDeleteHiyo Chadema ni ya baba-mkwe wake mzee Mtei, kupewa uwenyekiti mtu mwingine itakuwa ngumu, kwakuwa elimu yake ni ndogo haimruhusu kugombea uraisi, basi atakuwa mwenyekiti wa maisha......mkitaka ndio hivyo, hamtaki ndio hivyo......mzee Mtei hawezi kuharibu 'usinginzi' wa mwanawe.....ZIDUMU-FIKRA-ZA-MWENYE-CHAMA
DeleteMmmmm baba mkwe tena, basi kazi chama ni cha baba mkwe, sasa kumpa madaraka mtu kama Huyu au chama kama hiki si ni kujijtia kitanzini, maanake kutakuwa sio kuongozwa Bali kutawaliwa, mmmmm shughuli hili bara letu la giza. Na Tanzania yetu iko kwenye bara la giza,
DeleteNi hao hao ndio walosema atakaye mpokea Lowasa akapimwe akili, wamempokea, sina uhakika kama walishapimana akili..........
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteHahahahah,usiape!naipenda Chadema lakini wewe umenichosha.
ReplyDeleteTena utokomee kabisa, usije ukazani Wengi ni wajinga wajinga unajidanganya
ReplyDelete