PETER Lijualikali, Mbunge wa Kilombero, (Chadema) amesema akiwa mfugwa kwa yake kwa siku 79 katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam, aliteswa na kunyimwa haki zake, anaandika Pendo Omary.
Baada ya kutoka gereza la Ukonga amesema “kuishi gerezani unapaswa kuwa mvumilivu na mwenye busara. Kuna mateso ya kikatili ambayo ambayo wafugwa wanafanyiwa. Kuna wakati niliumwa maralia, daktari akashauri nipumzike. Lakini nilifanyishwa kazi ngumu na kuhatarisha afya yangu.”
“Askari Magereza saikolojia yao bado ipo kikoloni. Nimeshuhudia mtu anapigwa hadi anatambaa. Kuna harassment ambazo nilikuwa nafanyiwa. Nilipigwa sana.
“Gerazani kuna madaraja matatu, daraja la kwanza, la kati na la tatu. Kwa nafasi yangu ya ubunge nilipaswa kuwekwa daraja la kwanza. Ningekufa taifa lingepata hasara kubwa. Lingepoteza zaidi ya bilioni tano kurudia uchaguzi.
“Wakati haya yanafanywa kwa wafugwa wa kawaida, wezi wa meno ya tembo wakiwemo raia wa China wenyewe wanapewa huduma maalum ambazo ni nzuri, tena daraja la kwanza,” amesema Lijualikali.
Lijualikali amesema: “Uhusiano wangu na jeshi kama taasisi ulikuwa mbovu. Lakini uhusiano wangu na askari (mtu mmoja mmoja) haukuwa mbaya sana. Wengine walikuwa wananiambia walitumwa kunifanyia mateso na viongozi wao.”
Je wanasheria mnayasikia haya. Mtanzania haheshimiki. Tafadhali sana Tanzania kama nchi katiba na sheria za nchi zirudiwe tena na sasa. Ni kwa madlshi ya kumlinda Mtanzania mlipa kodi wa polisi na viongozi wote wa seriksli.
ReplyDelete