‘Msikubali Kuangushwa na Sisi Wachache, Nyinyi ni Wengi’ -Hussein Bashe


March 21, 2017 Mbunge wa Nzega mjini kupitia CCM Hussein Bashe amepost ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye maneno yaliyosomeka…

’Kama taifa wazee wetu walipoanzisha harakati za kudai uhuru na hatimaye tukaupata mwaka 1961 walikuwa na malengo‘

‘Upo uwezekano mkubwa kwamba sisi viongozi wa sasa tumewaangusha ninyi raia katika kufikia malengo ya waasisi wetu‘ –Hussein Bashe

‘Msikubali kuangushwa na sisi wachache, nyinyi ni wengi mna mamlaka na nguvu ya kututaka sisi kuwafikisha kwenye malengo ya Uhuru‘ –Hussein Bashe

‘Ni jambo la hatari kwa taifa inapotokea viongozi wakakosea na kutoka nje ya malengo, wananchi wakakaa kimya na kuogopa kuonya, kushauri, kukosoa au hata kukemea sababu tu ya woga au hofu.‘-Hussein Bashe

‘Tutakua tunajenga taifa la raia waoga msiingiwe na woga juu ya kudai haki zenu na kututaka sisi viongozi kutimiza wajibu wetu‘ -Hussein Bashe

‘Kwa kushindwa kwenu kutukemea au kutushauri tunapokengeuka sote tunaingia katika kundi moja la kuwakosea na kuwasaliti wazee waliopigania UHURU wa taifa letu. TUJISAHIHISHE‘ –Hussein Bashe
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. SIJUI ULIPATAJE UBUNGE MSOMALI WEWE"SAFARI YA MATUMAINI"

    ReplyDelete
  2. Msikubali kuyumbishwa na sisi wachache!Hahahaaa danganyana toto hiyo mnataka kumchuuza nani?Nyinyi wachache ndiyo mna mamlaka amri jeshi police wenye silaha kali vifaru ndege za kivita sheria haki utajiri mahakama ipo chini yenu nyinyi wachache sasa sisi mnaotuita wenig tupo mikono mutupu masikini mliotuhaidi wakati mnafanya bla bla... zenu za uongo wakati wa kampeni za uchaguzi tutaweza wapi?Tunamuachia Mungu lakini IPO siku nyinyi wachache mtalipa dhambi zenu hapa hapa duniani kwa tamaa na ukatili wenu mnaotufanyia sisi wenig

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad