Ni msala? Nyota wa sinema za Bongo, Irene Uwoya anadaiwa kusakwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni ili kutoa maelezo yake kwa kina kufuatia kifo cha kijana Fahari Colos katika ajali ya gari iliyotokea Masaki jijini hapa.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja, Uwoya anatakiwa kituoni hapo kwa vile, kifo cha Fahari kina utata wa simulizi kutoka kwa ndugu na kwa askari polisi waliokuwepo kwenye eneo la ajali.
Fahari alifariki dunia Machi 12, mwaka huu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili kufuatia ajali hiyo mbaya aliyoipata siku hiyohiyo. “Kama umesoma mitandaoni utakuwa umeona kuhusu ajali ya yule dereva wa bodaboda, sasa Irene Uwoya ana sehemu kubwa ya maelezo kutokana na ajali mpaka kifo cha yule kijana.
“Tumekuwa tukimtafuta kuanzia siku ya tukio lengo letu aje kituoni atoe maelezo maana na yeye ana sehemu ya maelezo muhimu. Lakini kama amezima simu au sijui ameiseti kiaina,” alisema afande mmoja na kutaka kusitiriwa kwa jina lake.
Amani juzi lilimtafuta Uwoya mwenyewe na kumuuliza kuhusu madai ya kutafutwa na polisi ambapo alisema:
“Mimi niko tayari kwenda kutoa meleozo yangu polisi, tena nitayatoa kwa uzuri sana. Kama wananitafuta safi sana.”
Kuhusu simulizi ya tukio hilo, Uwoya alisema:
“Machi 12, usiku nikiwa naelekea Masaki, kufika Colosseum Hoteli nilikuta ajali mbaya sana. Nilimkuta mkaka mmoja kagongwa na gari, yeye alikuwa na pikipiki.
“Nikasimama pale nikakuta polisi wapo na gari lao na ndiyo kwanza wanapiga stori tu, hawana habari watu wanaomba msaada.
“Niliwauliza polisi kwa nini mtu anakufa wanamuangalia tu? Wakajibu wao wafanyaje wakati hakuna gari la kumbeba! Nikawaambia gari lenu si hilo hapo? Wakasema haliwezi kumbeba, basi nikawaambia watu wampakie kwenye gari langu ili nimkimbize hospitali.
“Ile nataka kuondoka tu, wakaniambia nikachukue PF3 kwanza halafu niende hospitali, nikawaambia mtu anakufa nyie mnasema nikafuate PF3? Mimi sifuati PF 3, wakaniambia watapiga simu hospitali wasimpokee.
“Tukaenda na baadhi ya watu mpaka Hospitali ya Mwananyamala, kufika akapokelewa na tulikuta watu wa ajali wawili wamekaa karibu saa nzima.
“Niliumia sana! Tukaandikiwa vitu vya kununua kwa ajili ya majeruhi, kwenda nje hakukuwa na dawa, tukapata baadhi ya vifaa wakaanza kumhudumia! Baada ya muda difenda ikaja ikamchukua dereva wangu eti alikuwa anapiga kelele na kutukana wakati tulikuwa tunapiga kelele wamhudumie mgonjwa.
“Baada ya muda ndugu zake majeruhi wakajitokeza, mgonjwa akahamishiwa Muhimbili. Mimi nikamfuata dereva wangu. Kabla Sijafika kituoni akanipigia simu kwamba wamemuachia.
“Jana asubuhi (Machi 13) napiga simu kwa ndugu wa mgonjwa naaambiwa amefariki dunia. Niliumia sana kwa kweli. Sasa kama wanasema wananitafuta askari ili wanihoji sawa tu mimi nipo sana, nimejaa tele.”
Juzi, Amani lilimpigia simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Suzana Kaganda ili kumsikia anasemaje kuhusu kuwepo kwa madai hayo, lakini simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa