Msemaji wa Jeshi la Polisi Uganda Auawa kwa Kupigwa Risasi..!!!.


Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda Felix Kaweesi amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana. Taarifa zinasema Bw Kaweesi ameuawa baada ya gari lake kumiminiwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa anaondoka kwake nyumbani Kulambiro, Kisaasi kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kampala.

Walinzi wake wawili walioandamana naye pia wameuawa.

Bw Kaweesi aliteuliwa kuwa msemaji wa polisi Agosti mwaka jana.

Taarifa zinasema alikuwa njiani kwenda kuwahutubia wanafunzi katika chuo kikuu cha Uganda Christian University alipokumbana na mauti yake. Wanafunzi walikuwa tayari wamekusanyika ukumbini katika chuo hicho.

Miili ya watatu hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mulago.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad