Mwakyembe Ameliagiza Jeshi la Polisi Kumuachia Huru Msanii Ney wa Mitego.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego.

Waziri ameishauri BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo huo, na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.

Dkt. Mwakyembe amesema kuwa hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO na kumshauri msanii huyo auboreshe wimbo wake kwa kutaja watu wengine kama wakwepa kodi, wauza unga, wezi pamoja na watu wengine wasio na maadili.

Aidha Baraza la Sanaa Nchini(BASATA) lilitangaza kuufungia wimbo huo na kutoa onyo kwa wote wanaosambaza wimbo huo mitandaoni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad