Mwakyembe: Huwezi Kuwa Hakimu wa Kesi Yako Mwenyewe.....Ripoti ya Uvamizi Clouds Media Inamapungufu, Sitaipeleka Ngazi za Juu


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe leo amezungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma mara baada ya kukaribishwa rasmi Wizarani hapo..


Baada ya maongezi aliruhusu mwaswali ambapo moja ya swali aliloulizwa na wanahabari ni kuhusu ripoti iliyoachwa na Waziri wa zamani Nape Nnauye kuhusu uchunguzi wa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kudaiwa kuvamia ofisi za Clouds Media huku akiwa na Askari wenye silaha.


==>Haya ni majibu aliyoyatoa

"Wengi mnauliza nimeifanyia kazi gani ripoti ya Nape, mimi hiyo ripoti sijaiona na kama mwanasheria kwangu ni mwiko na sitapeleka taarifa ambayo haijakamilika.


"Kupitia vyombo vya habari taarifa imeeleza kuwa ushahidi ulitolewa na upande wa Clouds Media na mkakiri kuwa upande wa pili haukupatikana.

 

"Huwezi kuwa Hakimu kwenye suala lako wewe mwenyewe, kufanya hivyo ni ubatili kwahiyo hata mimi ningekuwa ni mwandishi wa habari ningesema hili jambo siliwezi kwakuwa linanihusu na mimi.


"Kanuni zinataka kusikiliza upande wa pili, sasa mmeshasema kitu kina upande mmoja alafu nimpelekee kiongozi wangu..NO, mimi kazi yangu ni kupata maelezo ya upande wa pili na nitapata.


"Hili jambo ni lakufa na kupona, yani niache kukutana na wakuu wa idara mbalimbali hapa kuhakikisha nakuza suala la sanaa na kuhakikisha vijana wetu hawaendelei kuibiwa nibaki kuhangaikia suala la ripoti.


"Mimi sikuapa kwa jambo hilo moja pekee lakini mimi ni mwanasheria mkongwe na nitahakikisha nalifuatilia lakini mimi sitaunda kamati katika jambo hilo.


"Lengo letu ni kuhakikisha hatutakuwa na matukio ya namna hiyo katika safari lakini tukitoka na kauli za papara tutakuwa tunajitafutia matatizo hapo mbeleni"
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwenye suala la Richmond, upande mmoja ulisikilizwa na maamuzi yakatolewa lakini kwenye hili suala ambalo liko wazi, Waziri anaongea alichoongea. Haya sasa na NECTA wamekataa kuwa na majina ya daudi bashite na Paul Makonda. watatuambia nini?? Mimi nadhani kwa uungwana tu, aliyekuwa waziri wakati Makonda anaomba udahili Muccobs abebe dhamana, Katibu mtendaji wa NECTA, Mkuu wa HESLB, na wale waliohakiki vyeti wakati wa zoezi la kuhakiki vyeti.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad