Nape Afanya Mkutano Kiana..Adai 'Niliikuta CCM iko Shimoni Nikaitoa Huko'


Nape Nnauye amezungumza na Waandishi wa habari akiwa juu ya gari lake leo maeneo ya St. Peter Osterbay Dar es salaam ikiwa ni saa chache kabla ya taarifa kutoka IKULU kutangaza kwamba nafasi yake ya Waziri wa Habari amepewa Dr. Mwakyembe, hii ni Sentensi hapa chini ya jinsi ilivyokua


"Nataka aliyeinua bastola hapa aje aseme ameiinua kwa sababu gani" - Nape Nnauye


"Nia ya mkutano wangu haikuwa mbaya. Nilitaka kuzungumza na waandishi wa habari lakini Polisi wanakuja kunizuia."- Nape


 "We have nothing to fear, but fear itself."- Nape


"Mnajua ni kiasi gani nimepigana kuirudisha CCM madarakani? Miezi 28 nimelala porini leo mtu anakuja kunitolea bastola. Jana nilisema kuwa kuna gharama za kulipa wakati unatetea haki za watu. Na nilisema kuwa nipo tayari kuilipa gharama hiyo. Sina kinyongo na serikali wala chama changu. Sikumuuliza Rais siku aliniteua na sitamlaumu kwa kuamua kuniondoa."- Nape


"Niliikuta CCM iko shimoni nikaitoa huko. Uzalendo wangu ndani wa CCM si wa kutiliwa shaka. Kina Kawawa walikuwepo wakapita, sisi tutapita, lakini tujiulize tutawaachia watoto wetu Tanzania ya namna gani?"- Nape


"Namshukuru Rais kwa mwaka mmoja alioniamini. Nampongeza kaka yangu Dkt Mwakyembe. Nawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe. Nawaomba mtulie maisha yaendelee. Nape ni mdogo sana kuliko nchi. Kuna mambo mazuri mbele hivyo tuiunge mkono serikali."- Nape


"Vijana naomba msimamie haki yenu"- Mbunge Nape Nnauye


"Mimi niliwahi kufukuzwa CCM kwa kusimamia nilichokiamini. Ili mbegu iote na kuchanua, sharti ioze kwanza."- Nape


"Namshukuru Rais kwa mwaka mmoja alioniamini. Nampongeza kaka yangu Dkt Mwakyembe. Nawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe. Nawaomba mtulie maisha yaendelee. Nape ni mdogo sana kuliko nchi. Kuna mambo mazuri mbele hivyo tuiunge mkono serikali."- Nape


"Nilitamani sana kuendelea kufanya kazi na ninyi waandishi wa habari lakini muda wa aliyeniweka umefika akaamua niondoke."-Nape


"Mimi niliwahi kufukuzwa CCM kwa kusimamia nilichokiamini. Ili mbegu iote na kuchanua, sharti ioze kwanza."- Nape
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Safi Sana magu.alijisahau huyo.hapA kazi tu..

    ReplyDelete
  2. Aibu kwa nchi nzima.
    Tulisema, Tulishauri sana wakati wa uchaguzi. Tumieni busara kumchagua kiongozi mwenye busara. Mwenye kujua Dunia inakwendaje. Msikivu, mwenye kuthamini wasomi wa Tanzania ambao ni asset number moja ya nchi hii. Bado tunaukoloni mambo leo.tunamtukuza mwekezaji anayetuchukulia mali zetu kawa almasi. Mtanzania msomi mpiga jasho kadharaulika. Mnakwenda Tafuta wawekezaji nje ambao hawana interest na nchi bali na mali za bure . Unampa Mjapani shamba alime viazi apeleke kwao, mtanzania amuuzie ushirika kwanza, sheria za kikoloni bado zinamlimbikiza mkulima Mtanzania na mnamyukuza mgeni aitumie nchi kuilisha nchi yake. Ni dharau ya namna gani. Ebu katiba mpya izungumzieni muikate hii mirija na chagueni viongozi bora wantakaojua namna gani ya negotiate madili ili Tanzania isimamie uchumi wake mwenyewe. Kwa kweli, Hatuna uongozi huru, safi. Hatuna sheria, Tunatawaliwa kama watu hawana elimu au akili.
    Ni AIBU KUBWA SANA NA POLE SANA. SASA MNAMTAMBUA LISU KWA NINI ALIDAI AWE kiongozi wa wanasheria Tanganyika. Ni kuwasikiliza Watanzania na si kuwaburuta .
    Mungu rudisha hadhi ya Nci, Mungu lete imani nchini, Mungu leta Amani Tanzania.Ni Nchi ya Umoja, si nchi ya watu waliolala.Haki itawale.Watu wawe na furaha badala ya kuwa waoga.

    ReplyDelete
  3. Hapa kazi tu. Sio kuleana leana. Au lelemama. Haya mambo ndio yanayuharibia nchi. Ya longolongo nyingi. Mara nimeitoa mbali ccm Mara shimoni. Raisi hayuko kichama yuko zaidi kiuongozi mambo ya chama eplekake hukoooo!!!!!! Hapa ni kazi na uongozi. Ndio wajibu aliokabidhiwa na Wanachi wake wapenda Amani na nchi yao kiujumla. Sio kulindana au kujuana kwenye maovu na kutupilia mbali mustakabali wa Taifa. Ukisema wewe ccm umeitoa mbali. Na wazee waleee wa zamani. Pamoja na hayati baba wa Taifa watasema nini?

    ReplyDelete
  4. Nape unarudi kuwatumikia wana Mtama ..Haya ni Maisha tuu. Nimemsikia Aitham amesema Nape kajiuzulu..Mimi namuamini huyu Kitoto. akasia wakataka kunufaika na skendo zenu ili tuibiwe matrilioni ya Dhahabu ikisadikiwa mchanga. Magu machele yamemcheza akastukia. Jamani hebu pumzika kwenu tuangalie ya ujenzi wa taifa na kufichua MAFISADI.NA UFISADI. ... FETI/CHITE/SHITE/KONDA VYOTE HAVITUSAIDIIII. WALA KULETA TIJA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad