Nape Atoa Neno Hili la Busara kwa Rais Magufuli na Serikali Yake..!!!!


Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema ataendelea kuwa mtiifu kwa Rais John Magufuli, Serikali na Chama cha Mapinduzi tofauti na maneno yanayosemwa mitandaoni.

Tangu alipoachwa kwenye mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, Machi 23, kumekuwa na taarifa nyingi feki kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuenguliwa kwake zikidaiwa kutolewa na mbunge huyo wa Mtama ambazo hata hivyo, amekuwa akizikanusha.

Akizungumza jana wakati akikabidhi ofisi kwa waziri mpya wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe katika ofisi za wizara hiyo mjini hapa, bila kutaja maneno hayo ya mitandaoni, Nape alisema ataendelea kumuunga mkono Rais katika dhamira yake njema ya kuleta mageuzi nchini.

“Heshima aliyonipa Rais ni kubwa mno na nitaendelea kumuunga mkono katika dhamira yake njema ya kuleta mageuzi nchini” alisema.

Alimshukuru Rais kwa kumpa dhamana ya kusimamia wizara hiyo kwa miezi 15 baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya kwanza. “Nitaendelea kutoa ushirikiano kwa wizara hii kwa sababu mimi ni mdau mkubwa wa sekta hiyo,” alisema.

Waziri Mwakyembe alisema ataendeleza mazuri yote yaliyofanywa na Nape katika kuimarisha wizara hiyo na atahakikisha wizara hiyo inakuwa ya mfano nchini.

Alimsifu Nape akisema katika kipindi kifupi alichokaa katika wizara hiyo amefanya mabadiliko na watu wameanza kuifahamu.

Nape aliondolewa katika nafasi hiyo siku moja baada ya kamati aliyounda kuchunguza tukio la kuvamiwa kwa ofisi za Clouds kumkabidhi ripoti.

Mara baada ya kupewa ripoti hiyo, Nape aliahidi kuikabidhi kwa mamlaka zake za juu akizitaja kuwa ni Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais lakini asubuhi ya siku iliyofuata aliondolewa katika nafasi hiyo.

Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na viongozi wengine wa wizara hiyo, naibu waziri, Anastazia Wambura, katibu mkuu, Profesa Elisante Ole Gabriel na naibu katibu mkuu, Nuru Millao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad