Nape Nnauye : Hili Likinishinda Hakika Nitajiuzulu


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesema endapo atashindwa kusimamia uhuru wa habari na vyombo vya habari nchini atakuwa hafai kubaki kwenye nafasi hiyo kwa kuwa atakuwa ameshindwa majukumu yake katika nchi huru

Nape ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumzia na kulaani kitendo kinachodaiwa kufanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, cha kuvamia chombo cha habari cha Clouds, akiwa na askari wenye silaha na kukifananisha kitendo hicho na kuinajisi taaluma ya habari.

Waziri huyo amesema amezoea kuona matukio kama hayo yanatokea kwenye nchi ambazo zimepinduliwa kwa bunduki lakini kwa nchi yetu si jambo jema kwenda kwenye vyombo vya habari na mabunduki mkononi.

"Tumezoea kuona matukio haya yanatokea kwenye nchi ambazo zimepinduliwa kwenda kwenye vyombo vya habari na mabunduki si sawa, kwa jambo hili tunataka kutenda haki tumsikilize Mkuu wa Mkoa ili tujue kwanini amefanya jambo hili". Alisema Nape

Kufuatia tukio hilo Waziri Nape ameunda tume yenye wajumbe takribani watano itakayoenda kumhoji Makonda na kutoa mrejesho wa kazi hiyo ndani ya masaa 24 ikiwa imeeleza sababu maalum kutokea kwa tatizo hilo.

Pamoja na hayo Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Dkt. Reginald Mengi amesema hawezi kutoa lawama kwa mtu yoyote mpaka pale ukweli utakapofahamika japokuwa ameonekana kukerekwa.

"Kwetu sisi hili ni jambo ni la hatari sana, linatuogopesha na linatishia maisha ya waandishi wa habari". Alisema Dkt. Mengi

Kwa upande mwingine Mengi amewasihi waandishi wa habari kutokuwa waoga kwa jambo lolote wanalopambana nalo ila wanachopaswa ni kufanya kazi kwa kufuata misingi iliyowekwa.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tatizo JPM hapendi kufanyakazi kwa AMRI, watu walishachonga sana basi wanyamaze waangalie MKUU atachukua hatua gani, badala yake WANAMLAZIMISHA afanye wanachotaka wao, HAIWEZEKANI

    ReplyDelete
  2. Unaunda tume ya watu watano ili iweje. Siasa.

    ReplyDelete
  3. binafsi namwona mh nape anaonyesha msimamo wake na anafanya kazi yake na ni haki yake kuzungumza kwakuwa aliteuliwa na Rais kwa kuona kuwa anafaa. kwann asimpe uhuru wa kufanya kazi yake? Nape jembe langu pambana usimwogope mtu kwani siasa za kumwogopa mtu kuliko hata Mungu zilishapita na wakati. i believe in you nape

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad