Noma Sana...Rais Magufuli Azidi Kumuumbua Dk Mwakyembe....!!!


Uamuzi wa Rais John Magufuli kufuta agizo lililotolewa na Dk Harrison Mwakyembe la kuweka sharti la vyeti vya kuzaliwa katika ndoa, unamuweka njiapanda waziri huyo wa sheria na katiba, huku wachambuzi wakisema hakufanya mawasiliano kabla ya kuagiza.

Mbali na kufuta, Rais amesema alishtushwa na agizo hilo kutokana na ukweli kwamba halikujadiliwa katika vikao vya Baraza la Mawaziri.

Mwakyembe, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, aliagiza ofisi za wakuu wa wilaya, viongozi wa dini na wa kimila kutofungisha ndoa iwapo wahusika hawana vyeti vya kuzaliwa kuanzia Mei mosi.

Alitoa agizo hilo juzi mjini Morogoro alipozungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na wawakilishi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) wakati akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo.

 “Serikali ya Dk John Magufuli imekusudia kukuza uchumi wa nchi kupitia viwanda. Hatuwezi kufanikiwa bila ya kuwa na takwimu sahihi,” alisema Mwakyembe.

Lakini jana, Rais Magufuli alifuta agizo hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuondoka Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kurejea Dar es Salaam, akisema kuwa sharti hilo linanyima haki ya kuoa na kuolewa kwa watu wasio na vyeti vya kuzaliwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad