Serikali imewasilisha bungeni mapendekezo yake ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya kiwango na ukomo wa bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2017/18 na inatarajiwa kukusanya na kutumia kiasi cha Sh 31.6 trilioni.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ameyasema hayo jana wakati akiwasilishwa mapendekezo hayo bungeni mjini hapa.
Pia, fedha za maendeleo zimeongezeka kutoka Sh11.8 trilioni mwaka 2016/17 hadi Sh11.9 trilioni mwaka 2017/18 sawa na asilimia 38 ya bajeti yote.
Bajeti za tanzania zimekuwa za kujifurahisha kusimama kusoma huku hali ya huduma za msingi zikiwa ni shida kwa wananchi
ReplyDelete