Oman: Mtanzania Auawa Kwa Kusukumwa Toka Ghorofani. Serikali Yetu ipo Wapi?

Assalam Aleykum

Katika matukio ambayo yanazidi kuonesha kuwa sisi watanzania labda hatuna haki ya kuishi au haki zetu binafsi hasa kwa nchi za kiarabu ambayo ndugu zetu hukutwa na majanga mazito huku balozi zikishrkiana na warab kuwakandamiza.

Juzi tarehe 14.03.2017
Msichana wa Kitanzania mkazi wa dar es salaam ambaye anafanya kazi za ndani Oman mtaa wa Bilad Ban Bu Alli, ambaye ana mwaka mmoja huko Oman.

Msichana huyu anaitwa Husna lakini alipofika Oman maboss zake wakambadilisha jina na kuitwa maryam, bado hatujajua kwanini wakifika wasichana nchi za kiarabu hubadilishwa majina yao.

Husna ambaye alkuwa na ugomvi na boss wake wa kike mzito ambao toka juzi bado tunafatlia kitovu cha ugomvi ninapota basi nitarejesha zaidi matokeo.

Ugomvi huo na boss wake wa kike ulipeleka husna kuishi kwa manyanyaso makubwa sana.

Siku ya tukio tarehe 14.03.2017 husna alipandsha juu gorofani kusafisha kama kawaida yake.

Boss wake wa kike baadae akamfata alipomfata ilitokea kutoelewana ndipo boss wake huyo alipomsukuma husna toka juu ya gorofa mpaka chini.

Alipodondoka chini husna yule boss akachungulia chini nadhani hakujua kama majirani watamuona.

Jirani alomuona ni rafiki wa husna ambaye nae ni mtanzania, boss yule kuona ameona akarudsha kichwa chake mbio mbio.

Baada ya watu kujaa kumtazama akiwa katika hali yake ya mwisho ya uhai wake, boss wake huyo ndipo aliposhuka chini wakampeleka hospital.

Hata alipofka hospital boss huyo hakutoa taarifa kwa ofisi ya agent ambao walompeleka husna oman wala hakutoa taarifa kwa balozi wa Tanzania nchini Oman mpaka jana.

Husna alifarki dunia akiwa njiani kupelekwa hospital.

Ndipo jirani huyo mtanzania alipompgia ndugu yake husna na kumtaarifu kifo cha husna, nduguye huyo anaitwa Zubeda Hassan.

Jirani huyo alipiga simu Tanzania kwa kusaidiwa na maboss zake mwenyew anaowafanyia kazi jirani huyo. Boss wa husna hakuweza toa taarifa popote hata kwa ndugu zake.

Visa vingi vinatokea nchi zote za kiarabu kwa manyayaso na mateso wanayopata ndugu zetu hasa wa kike ikiwemo.

Kulazimishwa kuingiliwa kimwili bila ridhaa yao,
Kuingiliwa kinyume cha maumbile
Kufanyishwa kazi ambazo hazikuwemo katika maelewano yao, ikiwemo kulisha ng'ombe, kufukiza vyumba ubani vyumba ambavyo havina kitu ikimanika kuea wanafukisha majini yao.

Dada mmoja kwa jina la Rukia mzanzibar ambaye sasa yapata miaka miwili toka kurudi saud arabia anasema, alikuwa akilazmshwa kuingiliwa kimwil na boss wake wa kiume, na baadae hata watoto wake wakiume aliposema kwa boss wake wakiume alimjibu na hao wape ni wanangu.

Wanapotoroka na kukimbilia ubalozini, ubalozi huwapigia simu maboss zao, kisha boss akija anawapa pesa na kumrudsha katika nyumba yake.

Kuna sero za siri nchi za kiarabu ambazo huwafunga wanaotorka kwa wajiri wao kwa mateso wapatayo.

UBALOZI WA TANZANIA OMAN

Katika sehemu inayolalamika na watanzania wanaoish Oman ni ubalozi wao.

Wafanyakazi wa Ubalozi kwanza wanajinasib kuwa na wao ni warabu, pia ushirikiana na warab kuwadidimiza watanzania, kesi nyingi zilizolipotiwa na watanzaia ubalozini huishia juu kwa juu.

Ubalozini wa tanzania oman wafanyakazi wengi ni wazanzibar, sio dhambi ila wanzibar sie tumesahau wajibu wetu na kugeuka taifa letu.

Tunamuomba Rais Magufuli na Rais Shein kuingilia kati matatzo ya watanzania waishio nchi za kirab hasa wafanyakazi wa ndani, ikibidi kuzuia kabisa wasiende uko mateso wanayopata siwezi andika yote.

Tuna balozi au tuna machozi??

Sisi hatuna haki ya kuishi??

Watanzania wanaonekana kama nyani mbele ya waraab huna pa kwenda kushtaki ukapata haki yao.

Mbaya zaidi ukifika uko hao maboss huchukua hati yako ya kusafiria na kuificha.

Ukiwa Tanzania wanakuhadi mshahara Rial 100 ambayo kwa Tsh. Ni sawa na laki nne hivi au laki tano lakini akishafika uko anabadilishiwa kibao na kulipwa pesa ndogo mno.

Hawana pa kusema wenye mamlaka wameziba maskio, hawasikii kamwe.

Anayewapa madaraka hawafatilii utendaji wao.

Magufuli ingilia kati roho ya husna na watanzania wote ambao wanakufa na kunyayaswa wanaharibiwa vibaya maisha yao.

Where Is Justice??

Ni kweli dunia hakuna haki??

Tuungane tuyapinge haya ndugu zangu, ndugu zetu wanateketea ifike wakati Nchi zingine zisiwachezee Watanzania maana wajue kuwa hawa serikali yao itafatilia na kuhakikisha haki inapatikana.

Magufuli namini unaweza, kama umaskini sio sababu wafanywe hivi.

Nawasilisha

Dada yake husna ambaye nas alipost hisia zake juu ya kuwawa kwa ndugu yake katika akaunti yake ya facebook

Source:JF/Brasy coco

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. IFIKE MUDA WATOTO WA KITANZANIA MULIDHIKE NA KILICHOPO TANZANIA.FANYA KAZI TANZANIA.

    ReplyDelete
  2. SAMAKI MMOJA AKIOZA SIO BAHARI YOTE JARIBUNI KUWATAJA MAJINA YA WATU WAHUSIKA SIO KABILA AU NCHI.SIDHANI KAMA SERIKALI YA OMANI ITANYAMAZIA SWALA HILO IENDAPO UCHUNGUZI UTAONEKANA.OMANI NI NCHI YENYE SIFA ZA HAKI YA BINADAMU.WAKO HOUSEMAID KUTOKA NCHI MBALIMBALI LAKINI TUJIULIZE KWANINI WATANZANIA TU WANAODHILILISHWA?WANAOKAA KWA RAHA NA AMANI KWA NINI HAMUCHAPISHI.TUNAOMBA SERIKALI YA OMANI ICHUKUE HATUA HIZI ZINAZOTANGAZWA KUHAKIKISHA HAKUNA DHULUMA INAYOTENDEKA KWA WATU WACHACHE WANAOHARIBU SIFA YA NCHI YA OMANI.SIO WARABU WOTE WENYE TABIA MBAYA.KWANI WAMASAI SIO WOTE WANACHUNGA NG'OMBE.TUJIHADHARI KUTAJA MAKABILA DINI NA NCHI KWA UJUMLA.NI BORA KUTAJA JINA LA MUHUSIKA.

    ReplyDelete
  3. Jamani kwanza jambo la kufanya ni kuhakisha hii habari ya msichana anae semekana kauwawa huko oman mji bani hassan hakuna majumba gorofa ni mi mji unaa nyumba ndogo ndogo .

    ReplyDelete
  4. HUO ULIKUWA NI UONGO MBONA HUYO BINTI ALIOKOLEWA NA YUKO HAI.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad