Ujenzi wa majengo 20 yenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya wanafunzi 3,840 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo kila jengo lina ghorofa nne umekamilika baada ya kuchukua muda wa miezi minane.
Suala kubwa nililojifunza katika siasa za Tanzania ni kuwa na kiongozi shupavu anayesimamia kile anachokiamini na kukiamua bila kujali kelele za wanasiasa wanafiki na wale wasioamini.
Ikumbukwe kuwa kuna wakandarasi walitaka kulipwa bilioni 100 katika mradi huu.
Kuna wengine walileta thread hapa na kuwaaminisha baadhi ya wana JF kuwa wataleta gharama kamili ya ujenzi lakini mpaka sasa ''wameingia mitini'' kwa sababu uwongo wao ulitumia lifti kuwafikia walengwa lakini kwa sasa ukweli unafika kwa kutumia ngazi.
Picha hizi pia zinatoa fundisho kwa wasioamini ambao pia wameainishwa kwenye vitabu vya Mwenyezi Mungu ndani ya Quran na Biblia.
Kwa wale wanaojua Quran wanaweza kuelewa maana ya maneno yangu kupitia verse 44 ya Surah Fussilat (41).
Kwa wale wanaojua Biblia wanaweza kuelewa maana ya hoja yangu kupitia Yohana 20:24.
Kuna msemo usemao, Kama hujui kusoma, hata picha huwezi kutazama?
Focus and perseverance is what separates winners from losers.
HAPA KAZI TU!
ReplyDelete