Polisi Dar Wakana Kumshikilia Nay wa Mitego


Jeshi la polisi kupitia kitengo chake cha habari na mawasiliano cha kituo cha kati (central) kimepinga kumshikilia Nay wa Mitego kwa sasa.


Kutokana na taarifa iliyopatiwa Bongo5 kutoka kwenye kitengo hicho zimesema kuwa rapper huyo kwa sasa bado anaendelea kushikiliwa na RPC wa mkoani Morogoro lakini leo au muda wowote anaweza kufikishwa Dar es Salaam kwa ajili ya kujibu mashtaka yake anayotuhumiwa nayo.

Wameongeza kuwa taarifa rasmi itatolewa pindi atakapofikishwa kituoni hapo.

Hata hivyo jana mwanasheria maaarufu nchini, Peter Kibatala alitoa taarifa kupitia mtandao wa Instagram kuwa Nay tayari amefikishwa katika kituo hicho cha kati.

Nay wa Mitego alikamatwa usiku wa kuamkia Jumapili hii mkoani Morogoro baada ya kuachia wimbo mpya uitwao Wapo unaikosoa vikali serikali ya Rais Dkt John Magufuli.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad