Rais Dr Magufuli Aipongeza Serikali ya Msumbiji kwa Kuwafukuza Watanzania..!!!


Rais Magufuli akiwa ktk ziara Mtwara amesema ni sawa tu kwa Serikali ya Msumbiji kwa kuwafukuza wahamiaji haramu.

Na amewataka watanzania warudi tu nyumbani kuna kila kitu ili tujenge nchi yetu.

Na ulivyokwenda ndivyo utakavyorudi kwasababu Serikali haikukupeleka Msumbiji na hata usafiri wanaopewa hauna sababu kwa sasa.

Amemshanga mtanzania kutoka Shinyanga kwenye dhahabu kwenda kuchimba madini Msumbiji.

Msumbiji ni marafiki wa Tanzania na wahamiaji haramu wasisababishe kuharibu mahusiano kati ya Tanzania na Msumbiji.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbona nasikia ni kawaida tu kwa wanamsumbiji kulima mashamba yao Tanzania na kurudi kwao Msumbiji?Nasikia hata wakati wa uchaguzi mkuu wa Msumbiji huwa wanaletewa mabox ta kupigia kura katika ardhi ya Tanzania. Nasikia huduma ya afya kaskazini ya Msumbiji ni dhaifu sana na hivyo ni kawaida kwa wanamsumbiji kutibiwa hospitali za Ndanda, Litembo na Mbesa ambazi zikondani ya Tanzania . Hii i

    ReplyDelete
  2. Niliongea ma mtanzania ambaye alilalamika kuwa hakuna fairneness kwani wasumbiji huingia na kufanya shughuli zao tz km wapendavyo ila watz nao wakiamini kuwa ujirani ni mwema nao wakienda kubenefit machimboni huko hupata hivyo visanga. Najua haifai wtz kuhujumu madini msumbiji. Ila sijajua kwanini ni halali kwa wanamsumbiji kulima ndani ya ardhi ya TZ. Serikali km haina habari basi ifuatilie jambo hilo. Na km si halali watz kunufaika na uchimbaji haramu msumbiji serikali iweke wazi km vigezo vipi vinahalalisha uhalali wa wanamsumbiji kulima na kutibiwa tz. Je wanapotibiwa wanatozwa ziada kama wageni? Km sivyo basi TZ iamke na kuuxa huduma za afya kwa wageni hao . Nawapenda wanamsumbiji sana ila naona diplomasia kwene hiyo mipaka kiasi fulani imelala usingizi hasa kwa upande wetu huu wa tanzania. Wanamsumbiji wameonyesha kuwa wanajali resource zao dhidi ya watz, bali TZ haijaonyesha hivyo bado ni dhama la bibi. Hayo ni maoni yangu.

    ReplyDelete
  3. Raisi hamzuii mtanzania yeyote kwenda au kuishi nje ya nchi. Anachosema ni kwamba, wasiwe illegal. Ni wahabesha wangapi tunawakamata na kuwarudisha kwao kila mwaka? Tunawakamata kwa sababu wako illegal? Kuna wahabesh wengi waliona makaratasi yote ya kuishi na kujihusisha na shughuri mbalbali Tanzania ikowemo kilimo ma ufugaji wanaendelea vizuri tu. Hawakamatwi kwa sababu wako na necessary documents zinazowaruhusi kujishughurisha na shughuri za kimaendeleo bila ya matatizo. Na kila nchi iko na sheria zake na procedures za mambo ya uhamiaji. Hivyo, mtanzania yeyote aliye nje kunyume cha sheria ajue risk zake.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad