Rais Magufuli Amsifia Mbunge wa Cuf,Amtaka Ahamie CCM Haraka..!!!


Rais Magufuli amempongeza Mbunge wa Mtwara Mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maftaha Nachuma kwa utendaji kazi wake.

Rais Magufuli amesema, ''Pamoja na kwamba CCM tuliteleza kidogo lakini Mbunge huyu ni mchapakazi kweli''.

Aliendelea kusema, ''Tunahitaji Wabunge wa aina hii, tumezunguka naye katika ziara yangu na kujionea kazi zake anazozifanya, Yeye anataka maendeleo ya wananchi wake''.

Alimalizia kwa kusema, ''Kwa kweli ninakupongeza, hongera sana. Una moyo mzuri hata sura nzuri''.

''Inawezekana sura ikawa CUF CUF lakini moyo wake ni CCM, Ningetamani siku moja ukahamia CCM, ningefurahi sana'' alisema Rais.

Mbunge Maftaha alimshukuru Rais kwa kumpa ushirikiano wa karibu katika kazi zake za kuwatumikia wananchi wa Mtwara Mjini.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wengine kuanzia mwanzo wa mwaka mpaka mmwisho wa mwaka na kesi tuu,kutwa mahakamani,saa ngapi watafanya kazi?

    ReplyDelete
  2. mi nahisi rais alimtania tuu jaman mbona mnapenda kuvalia njuga mambo ambayo hayana mbele wala nyuma duuuuuuuuuuuh

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad