Rasmi..Gwajima Aziunganisha Clouds Fm na Efm,Baada ya Jana Kufanya Yake kwa Ruge,Leo Anatuma kwa Majizo wa EFM...!!!


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Bishop Josephat Gwajima amesema kuwa leo hii atatembelea kituo cha redio cha Efm pamoja na TVE kwaajili ya kuwapa pole wana tasnia ya habari kwa yaliyotokea.

Ijumaa iliyopita kituo cha Clouds kilivamiwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na askari wenye mitutu kitendo kilichopingwa na wadau mbalimbali wa habari.

“Kesho Tarehe 23/03/2017 Saa nne kamili asubuhi, nitatembelea Ofisi za EFM na TVE ili kuwapa pole wana tasnia ya Habari kwa yaliyotokea.” aliandika mchungaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Askofu huyo jana alitembelea kituo cha Clouds kwaajili ya kutoa pole kwa yaliyotokea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad