Rungwe Amkalia Kooni Paul Makonda Sakata la vyeti


Rais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe Spunda amemshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujitokeza hadharani na kutoa ufafanuzi juu ya utata wa jina lake unaozidi kuvuma mitandaoni
*
Utata huo unadaiwa kutokana na mkuu huyo wa mkoa kutumia cheti cha mtu mwingine cha kidato cha nne kujiendeleza kielimu.
Rungwe ametoa ushauri huo leo kupitia kipindi cha maswali na majibu cha Kikaangoni , akimsisitiza Makonda kuweka ukweli mezani na kuacha kupiga chenga za mchangani kwa maana akiendelea kukaa kimya watu wanazidi kuamini uvumi huo. "Namshauri Mkuu wa mkoa ambaye ni kama mwanangu, atoke azungumze ili kumaliza huu utata wa vyeti, asimsumbue Rais ana mambo mengi" Amesema Rungwe
*
Pia, amemtaka kuacha kulia madhabahuni, kwakuwa hilo halitamsaidia kwa kuwa kulia siyo jibu, na atambue kuwa ofisi hiyo aliyopo sasa siyo yake bali ni wananchi, hivyo kila alichokikuta atakiacha. "Siku moja nafungua 'ipad' yangu namuona Mkuu wa Mkoa analia mbele ya kanisa halafu mchungaji anambembeleza kama mjukuu wangu, mimi namwambia kulia kwake hakusaidii kitu yeye anapaswa kusema ukweli tu kama hilo jina siyo la lake halisi ila ni la kisanii sisi tutamuelewa". Alisema Rungwe
*
Aidha Rungwe aliendelea kufunguka kwa kumtaka Makonda kuacha kung'ang'ania nafasi ambazo anastahili katika nafasi hiyo huku akimpiga kijembe kuwa mwanaume hachagui kazi aende akabebe hata zege kama hana ujuzi wa kufanya.
*
Alimaliza Hivyo Ndugu Rungwe.. Nini maoni yako mdau.. Unamuunga mkono Rungwe au unapingana naye???
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Naunga mkono. Ccm acheni kuichezea nchi na sheria itfuatwe.huu si mchezo. Hii ni halisia ya sheria za nchi na usawa. Mtawatumia wanamuziki wasio na elimu mbadala, lakini mjue hii ni sheria, usawa, na hadhi ya watanzania. Ni mkakati wa viongozi wa ccm walioshindwa kukabili uingizaji wa madawa na kuchukua njia mkato. Hakuna njia mkato bali sheria tu. Acheni ncezo wa kamali na kuchezea nchi na watu kama mali zenu.

    ReplyDelete
  2. mzee rungwe kanena ukweli kabisa awache kubabaisha na kulia ovyo mwanaume halii kama kuna ukweli basi auanike awazibe midomo wenye kelele ila nasema hivi huyu sasa sijui nimuite bashite au makonda bwana unatutatiza toa tu vyeti wacha kulia ovyo au kumtumia TID kuobgea kwenye media unataka sympathy frm raisi tia vyeti kitu kimoja ujuae kwamaba hakuna mtu anaipenda kuharibika kwenye madawa ya kulevya ila bob ulikosea sana unataja watu ovyo ovyo bila ubakika wowote na pale uliposhindwa wewe na huyo siro sijuo nani munasingizia watu munawalazimisha watu waonge uongo eti ndio mimi natumia we kweli ni wa wapi? watumiaji na wabebaji na wauzaji hawafichiki mfano HUYO TID YES NI MTUMIAJI NA NDIO MANNA KAKUBALI NA KUKU SUPPORT KUKANDAMIZA WASIOTUMIA KUSUDI UWAHARIBIE MAJINA kuwa kiakili au ndio hayo masifuri yako yanakuendesha ufanye ujinga wako hapo ulipo sio darasani mjomba amka

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad