Sakata la Askofu Gwajima na Polisi Lachukua Sura Mpya, Hiki Ndicho Kimetokea...!!!


Wakili Peter Kibatala amesema polisi wamepiga picha nyumbani kwa Askofu wa Kanisa la Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima.

Kibatala ambaye ni wakili wa Askofu Gwajima amesema jana kuwa mbali na kupekuwa na kupiga picha kila kona walikwenda katika kanisa lake lililopo Ubungo.

“Waache wafanye yao na sisi tutafanya yetu kisheria. Kwani hatuwezi kuwazuia Polisi kufanya shughuli yao na baada ya kumaliza na sisi tutajua nini cha kufanya,”amesema Kibatala.

Aidha Msemaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, David Mngongolwa amesema “Gwajima alikwenda jana kuripoti kama alivyoamriwa kufanya hivyo, baada ya kuripoti askari walimchukua na kwenda naye nyumbani kwake wakakaa kwa dakika zisizozidi sita na kuondoka naye.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda amesema hana taarifa za kukamatwa kwa Gwajima kwa maelezo kuwa alikuwa katika kikao.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NYIE MWACHENI TU HUYU/KAYAKOROGA ATAYANYWA SHINANDANA NA SERIKALI KISHA KWA KUIZUSHIA UZUSHI MTUPU WW NANI..ANABAHATI HUYU KTK UTAWALA NYERERE R.I.P. SAIVI TUNASHAMSAHAU...DOMO KAYA..WACHUNGAJI FAKE KM HAWA DAWA YAKE MNAIJUA CCM KIMYAKIMYA MTU ANAOZA...KM YULE

    ReplyDelete
  2. Wewe uliye Comment hapo juu sidhani kama una akili timamu,nyie ndo akina Bashite kabisaaaaaa,kumbe mpo wengi eeeeeeh? Sasa hapo CCM na Gwajima wapi na wapi? Punguza mihemko,changia point,very idiot!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad