Sakata la Kugushi Cheti la Makonda Lachukua Sura Mpya,Meya wa Ubungo Kupitia Ukawa Aibuka na na Haya Mapya..!!!


Asalaam Allleikhum wana Dar es salaam. Baada ya Salamu, naomba nitoe shukrani kwake Mwenyezi Mungu wa mbingu na ardhi, anayetupa pumzi ya kuhema bila malipo, yeye atoae uzima kwa vinavyo onekana na visivyo onekana, sifa na utukufu virudi kwake maana hakuna kama yeye.

Leo ninarudi ubaoni nikiwa na majibu kwa Wananchi wote waliopo Dar es salaam na nje ya Dar es salaam mliopata kunipigia na kunitumia sms juu ya *"KASHFA YA KUGUSHI VYEKI"* Inayo mkabili moja wa viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam.

Mosi, Mimi kama nguzo na Kiongozi mmoja wapo ninae unda uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam ninajibu kwa niaba yangu au kwa ukaribu wa mashirikiano baina ya serikali kuu na serikali za mitaa Dar es salaam, kwa maana zipo namna nyingi tunahitaji kushirikiana na uongozi wa serikali kuu Dar es salaam, kwa hiyo lolote kuhusu Dar es salaam yanatuhusu sote ndiyo maana hatuwezi nyamaza.

Pili, ya kwamba Ofisi ya Mkoa Dar es salaam, ikikumbwa na kadhia na kashfa kubwa kiasi hiki kwa namna yeyote sisi wawakilishi pekee wenye dhamana Dar es salaam kwakuwa sisi ndiyo tumechaguliwa wengi kuongoza Dar es salaam, kwa madiwani wengi, wabunge wengi; kwa hiyo basi ukinajisi ofisi ya mkoa kwa kuwa na kashfa ya "UHALIFU WA KITAALUMA" basi ni sisi viongozi wa kuchaguliwa na wananchi tunapaswa kutoka na kuwasemea Wakazi wa Dar es salaam kwakuwa dhamana hiyo tunayo sisi.

Sisi Viongozi wenu tupo imara na tuna wahakikishia kuwa DAR ES SALAAM, haita kaa kamwe iongozwe na "KILAZA" na si tu KILAZA bali "MUHALIFU WA TAALUMA". Njia pekee ya Mameya, wabunge ma Madiwani Dar es salaam kutoa ushirikiano na serikali kuu ni moja kati ya haya yafanyike.

1. Utolewe ufafanuzi juu ya kashfa hiyo kwa kiongozi muhusika kujitokeza na vyeti vyake vyote na kuvianika hadharani.

2. Serikali imsafishe haharani kama wanayo taarifa nyingine zaidi ya hizi walizonazo wananchi, au serikali imchukulie hatua kama muhalifu mwingine yoyote bila kujali cheo chake, chama chake au ukaribu na mkuu wa nchi.

Vinginevyo sisi kama viongozi wa Dar es salaam tumefedheheshwa sana Kusikia kashfa hiyo ya kugushi vyeti kwa kiongozi wa Mkoa wa Dar es salaam, na bila ya unafiki inatuwia ngumu kufanya naye kazi yoyote bila ya kupata ufafanuzi binafsi wa muhusika kwakuwa viongozi wenzie Tumeathiliwa kisaikolojia......hivyo kila anachokifanya tunakihusisha na kufeli kwake na kugushi kwake vyeti vyake vya taaluma.

Kwa mfano .....
1. Tangu Mwaka jana mwezi march ajawahi kuitisha kikao cha mashauriano cha mkoa wa Dar es salaam; na ikumbukwe vikao vya mashauriano mkoani ni vya kisheria na yeye ni mwenyekiti wa vikao hivyo, kwa mwaka vinapaswa kukaliwa mara nne. Je tunajiluza kama kazi yake namba 1 anashindwa kuifanya anajua kweli wajibu wake? Na kama hajui, je ni kufeli na kugushi kwake ndio kumepelekea kushindwa kumudu majukumu yake hayo?

2. Tangu mwaka jana mwezi march hajawahi kuitisha kikao cha bodi ya narabara na ilhali yeye ni mwenyekiti. Wabunge na Mameya ni wajumbe, hii ni kazi yake muhimu katika kazi zake kuu tatu, je alikuwa hajui wajibu wake au ni kufeli na kugushi kumepelekea kushindwa kumudu majukumu yake?

3. Waziri mkuu yupo mkutanoni anaongelea Maswala ya umeme, waliopo mbele na wafanyakazi wa TANESCO,wewe unaongelea SHISHA, kama si UBASHITE ni nini?

Mwanzo wakati anafanya hivyo tuliona kawaida ila baada ya haya yote tunajiuliza huenda kufeli kwake na kugushi vyeti kulisababishia yote haya.
Na mengine mengi tu, ambayo kimsingi sisi kama viongozi wa UKAWA Dar es salaam , Mameya, Wabunge na Madiwani tunasitisha mashirikiano na ofisi ya mkuu wa mkoa mpaka pale tutakapo pata usahihi wa kashfa hii kwenye ofisi ya mkoa, ili tusiendelee kuathirika kisaikolojia ni vyema kiongozi binafsi au serikali itufumbulie fumbo hili, ambapo tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, haijawahi kuwa na kigugumizi isipokuwa kwenye jambo hili.. kunaniii?

Wenu katika ujenzi wa Taifa
BONIFACE JACOB(Senior councilor),
KATIBU WA MAMEYA CHADEMA TANZANIA,
MJUMBE KAMATI KUU CHADEMA,
MSTAHIKI MEYA UBUNGO.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  2. Hata wewe ni jipu,haya ya vyeti yalitakiwa yatolewe ufafanuzi mara tu alipochaguliwa kuongoza wilaya ya kinondoni katika awamu ya 4 maana mlikuwa mnamuongelea sana.

    ReplyDelete
  3. maneno ya mkosaji tu hayo aliyepewa kapewa na kamwe haiwezi kuponyeka na binadamu yyt hadi mungu atake hakuna jipya hizo ni kelele za mbwa anaelinda nyumba haziwezi kumkosesha mfuga mbwa usingizi

    ReplyDelete
  4. Makonda anaweza kuwaziba vinywa hawa wanaomsingizia kuwa ana yeti fekikwa kuvianika vyeti vyake ili kila moja avione, hilo litakuwa jambo la mana kuliko kulumbana. Vyeti bila ya shakaanavyo kwahivo avianike ili wabaya wanafiki wakome kusingizia maovu. Hayiingii mkuu wa mkoa vila ya vyeti vya masomo yake. Hii ni husuda tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad