Kuna vitu huwa sielewi hapa. Mwaka fulani ilitajwa orodha ya mafisadi wa elimu waliokuwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika wa Bunge alikuwa Marehemu Mzee Samwel Sita (Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake mahala pema peponi, Amina), Spika akaingilia kati kusema PhD ya Dr. Mathayo David ilikuwa halali hivyo katajwa kimakosa, ila wengine wote waliobaki hakuwasemea mf, akina Dialo (Dr.), Merry Nagu (Dr.) nk. Lakini nakumbuka baada ya Mzee Sita kusema hivyo, TCU immediately walitoa tamko, ya kwamba wao ndio wenye mamlaka ya kusema kama Degree ya mtu fulani ni feki ama vinginevyo na baada ya hapo hata vile vijarida na yule bwana aliyekuwa kinara wa ile scandal sijui walipotelea wapi.
Nirejee kwenye hii scandal maarufu ya Daudi Bashite Vs Paulo Makonda, tunazo taasisi zetu nyingi kuanzia hizo za kitaaluma alikopita huyo Ndg, anza secondary school both O level and Advanced Level, kuna walimu waliomfundisha, na baraza la Mtihani NECTA nk. Twende kwenye Chuo alichosoma tena hivi majuzi tu kote huko vyombo vya kiuchunguzi vinapajua na panafikika na sio wala nje ya nchi na hakuna gharama kihivyo.
Binafsi naamini kama hiyo ni kweli ni swala la muda tu, let us wait and see, lakini kama ni longo longo kwa nini tunapoteza muda wetu.
Kuna mkubwa mmoja katika taasisi moja hapa nchini, yeye alisema ana PhD, Chuo alichopata hiyo Degree yake SA, watu wakaanza kusema sema alikimbia mwenyewe ofisi, ingawa kiutendaji alikuwa mzuri kabisa na ni kweli aliwahi kufanya hiyo Degree yake huko SA ingawa haiku- materialize.
Kumbe basi ni swala la muda tu, maana tumeshudia watu wengi wakifutika humu makazini kama upepo na wengine wakistafu gafla, ukiuliza unaambiwa vyeti vina utata, hivyo basi kama jamaa naye kuna hila ipo siku ataondoka tu. Binafsi naamini kwa hizi kelele ambazo zimepigwa kuhusu Bashite vyombo vya uchunguzi vilikwisha maliza kukusanya taarifa kuanzia kijijini Kolomije, shuleni msingi na sekondari na hadi chuo.
Nikimwaangalia Makonda bado ni kijana kuliko mimi, lakini mimi nikienda shuleni kwangu msingi bado wapo walimu walionifundisha primary pale kituoni zaidi ya 20 yrs ago, ingawa wengine wamehama na wengine kustaafu, lakini hata wasipokuwepo taarifa zinapatikana tu. Sasa sembuse huyo, Jamani Sefue Ombeni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi aliandikwa na Gazeti moja tu, akatoka akakanusha kwa nguvu zote juu ya ile taarifa na vitisho vya kwenda mahakamani na kudai fidia, mbona baada ya muda mfupi aliondoka. Ingawa sijui kama kuondoka kwake kulitokana na ile habari iliyooandikwa na lile gazeti, lakini walau ndio taarifa pekee ya mwisho iliyokuwa na ukakasi kumuhusu yeye binafsi na sio taasisi.
Mamlaka ya uteuzi wa Mkuu wa Mkoa (RC) ambayo ni Rais, ina mikono mirefu na mipana, ina macho mengi na yenye nguvu ya kuona kila sehemu, tuipe ushirikiano chanya katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku likiwemo hili la Daudi Bashite nadhani itatoa majibu nasi tutayaona hata pasipokuambiwa. Hizi kelele nyingi kupita kiasi zinaweza hata kuwapoteza na kuipuuzia hii taarifa kwa kuzani ni kelele za watu walioguswa na utendaji wa Ndg Makonda hasa kwenye dawa za kulevya.
Katika utendaji kazi wake hasa kwa siku za hivi karibuni kama Mkuu wa Mkoa Ndg Makonda sote tunajua amegusa eneo la watu wenye nguvu ya pesa chafu, majuzi nimeona comment ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif, juu ya hii vita, kila mtu anajua nguvu ya hao watu, wanaweza fanya jambo lolote hasa kwa watu wa kawaida kama akina RCs nk, maana kuna nchi tunaambiwa hata President anaweza kupinduliwa na drug dealers, hivyo mimi kwa kutambua uwezo mkubwa wa watu walioguswa na RC Makonda hivi karibuni, nitakuwa wa mwisho kuamini kila baya linalozungumzwa kuhusu Makonda kwenye social media na kwingineko mpaka vyombo husika vitakapo toa taarifa aidha in public ama tukaona vitendo kama enzi ya kina Sefue nk. Mwanzoni kuanzia kule Bungeni tuliambiwa ana majumba ya Gorofa ndani mwaka mmoja nk, leo havisemwi tena.
Mwisho kabisa, natamani kuona vyombo vyetu (Responsible Institution) zikifanya kazi yake kwa umakini na kutoa taarifa sehemu husika kwa utekelezaji na sio vinginevyo. Ahsante
Nimeipenda saaana article hii naamini aliyeiandika ana high level of thinking capacity...........well said ndugu
ReplyDelete