Samatta Afunguka Haya Mbele ya Waandishi wa Habari Kwenye Mazoezi ya Stars


Leo March 22 jioni, kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars kilifanya mazoezi kwenye uwanja wa Taifa kwa ajili ya maandalizi ya mechi zake mbili za kimataifa dhidi ya Burundi pamoja na Botswana.

Kabla ya kuanza kwa mazoezi, waandishi wa habari waliojitokeza kushuhudia Stars akifanya mazoezi walipata fursa ya kuzungumza na nahodha wa Stars Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anakipiga barani Ulaya kwenye klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Waandishi walitaka kujua mambo kadha wa kadha kutoka kwa Samatta ambaye bila shaka nae akafunguka kama ifuatavyo…

Baada ya kufanya vizuri tangu alipojiunga na KRC Genk, kuna offer yoyte rasmi kutoka vilabu vikubwa ambayo imeshamfikia?

Niko pale na nina furaha kuwa pale, kama kuna lolote litatokea ni masuala ya muda tu.

Tanzania imekuwa ikiporomoka kwenye nafasi za viwango vya FIFA, kama nahodha anadhani tatizo liko wapi?

Sio suala la nahodha ni jukumu la wachezaji wote, viongozi na watanzania. Imefika kipindi tuangalie kwamba tunaelekea wapi, isiwe wengine wanacheka wakati wachezaji wanaumia, ni suala la watanzania wote kutengeneza misingi kwa pamoja kwa ajili ya timu ya taifa kwa sababu inapokuwa inaporoka halafu tunatupiana lawama haipendezi.

Alikuwa anatamani club yake (KRC Genk) ikutane Mnchester United kwenye robo fainali ya Europa League ili atimize ndoto yake ya kukanyaga Old Trafford, baada ya ratiba kutoka na timu yake kupangwa na Celta Vigo amesjisikiaje?

Ni mechi nzuri pia kwa kuongeza uzoefu, sio game ndogo Europa kucheza na Celta Vigo

Baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani lipewa eneo la kiwanja kama zawadi na wadau nchini kwa ajili ya kujenga kituo cha soka cha vijana, mpango huo umefikia wapi?

Siwezi kuanza kujenga kwa sasa kwasababu ntakuja kufa njaa badae, itafika kipindi kila kitu kitakuwa sawa muda utaongea hilo ni lengo langu toka kitambo sana na nitalifanya kwa sababu ni lengo ambalo nilijiwekea mwenyewe.

Kukosekana kwa Thomas Ulimwengu kwenye timu ya taifa kwa ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa kutaiathiri vipi timu ya taifa?

Nitam-miss ni rafikiangu lakini vile vile tulikuwa tumetemngeneza uwiano mzuri kwe ye timu lakini kama mwanajeshi muda mwingine inabidi ushirikiane na watu wengine sio lazima awe mtu ambaye umemzoea . najua hata Tanzania wachezaji wengine na mashabiki pia watam-miss lakini ana majeruhi na hawezi kutumika inabidi tulielewe hilo.

Maoni yake kuhusu kocha wa taifa wa sasa Salum Mayanga

Alikuwa kocha msaidizi kipindi cha Mart Noij na tulikuwa tunafanya kazi pamoja kwenye timu ya taifa tunafahamia na anawafahamu wachezaji wengi wa kitanzania wa timu ya taifa.

Anawasaidiawachezaji wa Tanzania kupata nafasi za kucheza soka la kulipwa nje ya nchi?

Nashindwa kujibu moja kwa moja kwa sababu kwa sasa naweza kuonekana kama natafuta sifa ya kuonekana nasaidia wengine nafikiri liachwe labda wachezaji wanaweza kuongea wenyewe japo hatujafanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini itafika kipindi itakuwa rahisi.

Anajisikiaje pale jina lake linapotajwa na wasanii kwenye nyimbo zao?

Kuna wasanii wengi walikuwa wanataja jina langu kwenye nyimbo zao tangu nikiwa TP Mazembe labda zilikuwa hazisikiki au watu walikuwa hawatilii maanani kwa sababu Samatta alikuwa bado yupo Afrika. Najisikia furaha kwa sababu nahisi watanzania wenzangu wananipa sapoti na wanajali kile nachofanya , wasanii wote mimi ni washkaji zangu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad