Stooop..Snura Mushi Akataa Watoto Wake Kumuangalia...!!!


Kama mama, kama mtoto hilo halipo kwa Snura. Mrembo huyo amefunguka kuwa hataki watoto waje kuwa wanamuziki kama yeye.

Akiongea na gazeti la Risasi, hitmaker huyo wa ‘Shindu’ ambaye kwa sasa ana watoto wawili amesema maisha ndiyo yaliyomsababisha yeye aingie kwenye fani hiyo lakini hapendi watoto wake waingize mguu kwenye tasnia hiyo.

“Nafanya muziki kwa kuwa natafuta hela. Maisha yamenifanya niingie kwenye fani hii lakini siyo kwamba ndiyo naipenda mpaka niwarithishe na wanangu. Sitaki kabisa wawe kama mimi, ukiniuliza kwa nini jibu langu ni hilo,” amesema Snura.

“Sina sababu ieleweke hivyo tu, nashukuru Mungu wanangu nao hawana muda na fani hii na ninapenda waendelee kuwa hivyo kwani sipendi wanangu wafanye kazi hii,” ameongeza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad