Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Chama cha Democrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani Mhe. Frederick Sumaye ameiomba serikali kusimamia misingi ya demokrasia katika kutatua malalamiko ya wananchi na kusimamia ustawi wa jamii ya Watanzania.
Mhe. Sumaye ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kama serikali itafanyia kazi malalamiko na mapendekezo yanayotolewa na wananchi ni wazi taifa litafikia malengo yake iliyojiwekea ya kupunguza hali ya umasikini na kuongeza pato la taifa kwa ujumla.
Wakati huo huo Mhe. Sumaye amewaasa watendaji wa serikali kutumia vizuri misaada inayotolewa na nchi wahisani ili kuhakikisha fedha za wananchi zinazotumiwa katika ulipaji wa madeni hayo zinakuwa na manufaa kwa watanzania wote hasa wale wasiofikiwa na huduma muhimu za kijamii.
Mr. Zero tulia mpaka 2020 mtamwelewa tu Magufuli wetu yaani anatukosha nchi ilioza ikaozeka leo mnatetea majungu mmeungana na wazungu wa sembe kumng'ang'ania makonda hamuoni hii ni vita baina ya makonda wa wauza madawa ya kulevya ni kama vile mnawasaidia wauza sembe kuuzima huu mziki wa makonda ili waendelee kuwamaliza vijana kwa tamaa zao za utajiri huku taifa linateketea
ReplyDeleteHeh! Mr. Ziro kumbe yupo, wanaibuka kwa vipindi kama mvua tehetehe
ReplyDeleteTumaye... Mimi nilisikia umelazwa. Je ulizungumza haya Kitandani au mtandaoni manake Sielewi au Sifahamu.. Ndio wale yule.. Kumbuka samba hata Darrasa amesema unatembea bila blek what do u expect? Kifoooooooooooo. bwana akupe uzima.
ReplyDeleteTumaye... Mimi nilisikia umelazwa. Je ulizungumza haya Kitandani au mtandaoni manake Sielewi au Sifahamu.. Ndio wale yule.. Kumbuka samba hata Darrasa amesema unatembea bila blek what do u expect? Kifoooooooooooo. bwana akupe uzima.
ReplyDelete