Sumaye Aisifu Serikali ya Awamu ya 5 kwa Maendeleo...!!!


MWENYEKITI wa Kanda ya Pwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fredrick Sumaye ameupongeza uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa hatua mbalimbali za kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali nchini na hususani katika Jiji la Dar es Salaam.

Aidha, Sumaye ambaye alishika wadhifa wa Waziri Mkuu kwa miaka 10 katika utawala wa Serikali ya Awamu ya tatu ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia uchaguzi uliofanywa na chama hicho na yeye kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kanda hiyo, makamu mwenyekiti wa kanda hiyo akiwa ni Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea na Mweka Hazina akiwa Ruth Mollel ambaye pia ni mbunge wa chama hicho kupitia Viti Maalumu.

Kanda ya Pwani inaundwa na mikoa ya kichama ya Pwani, Ilala, Kinondoni na Temeke.

“Kwa Dar es Salaam, serikali imechukua hatua nyingi za kuleta maendeleo, kwa kweli sisi wapinzani inabidi tuwapongeze na kuiunga mkono serikali hii ya awamu ya tano kwa namna inavyojitahidi kuleta maendeleo natoa wito kwenu tushirikiane nao tuache kugombana nao"

Aliwaagiza wabunge, mameya, madiwani pamoja na wenyeviti wa mitaa ambao miradi mbalimbali imetekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano wawaelimishe wananchi namna ya kuwa karibu na miradi hiyo.
Sumaye alisema baada ya kanda hiyo kupata viongozi masuala ambayo watayafanyia kazi ni pamoja na kusimamia maslahi ya wananchi ili waweze kupata maendeleo, heshima utu utawale na kuangalia ukuaji wa demokrasia.

Alisema kazi ya vyama vya upinzani ni kuishauri serikali iliyoko madarakani na kushirikiana nayo kuleta maendeleo.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ati watu wanasema ulipata kuwa katika ngazi ya uongozi kwa muda vile. Je ni kweli ? na ngazi ipi?

    ReplyDelete
  2. Ati watu wanasema ulipata kuwa katika ngazi ya uongozi kwa muda vile. Je ni kweli ? na ngazi ipi?

    ReplyDelete
  3. Ati watu wanasema ulipata kuwa katika ngazi ya uongozi kwa muda vile. Je ni kweli ? na ngazi ipi?
    Mimi siamini..!!! na kama ni kweli itabidi ujieleze.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad