Kuna upuuzi unaendelea mitandaoni na wabana pua kwamba oooho Trump ampongeza rais wetu kipenzi. Ikulu ya Marekani ndio inaandika kiingereza kibovu vile na inatumia wasapu siku hizi badala ya njia sahihi toka White House Kiingereza kile kina sura na mfanano kabisa wa mwandiko wa ndugu yangu Humphrey Polepole, labda siku hizi amekuwa mwandishi na msemaji wa Donald Trump wa Chamwino pale Dodoma...Lakini Trump yule wa Marekani sijui kama anajua kuwa kuna Tanzania ya Magufuli, ninachofahamu anajua kuna Afrika ya Nyerere, Nkurumah, Mandela, Lumumba, Mugabe, Museven nk.....
Hotuba ya Donald Trump wakati akisaini sheria ya kuzuia wahamiaji kuingia nchini mwake hakuna mahali alipotamka neno Magufuli, wala hakuna alipomsifu... Nilifuatilia hotuba ile, lakini mtandao wa radio ya Ufaransa ya kiswahili umechomekea maneno hayo nakufanya habari kuwa tofauti kamia propagsnda za aona hii bisa, Ukweli Rais wetu tutamsifu wenywe kwa mazuri yake sio kwakutumia propaganda za aina hii, Bahati mbaya vyombo vya habari vya kimataifa vinavyotumia lugha ya kiswahili vingi vimejaa watanzania wenye ushabiki wa vyama (makada) ambao muda mwingi wanatumika vibaya.
Rais asifiwe kwa mazuri yake mfano mimi namuunga mkono kwa 100% Zanzibar ibebe msalaba wake, Muda wa kubebwa Zanzibar umekwisha ilipe deni la tanesco ili shirika letu liweze kujiendesha... Tumewabeba kwenye bajeti ya Masuala ya Muungano ambapo Bajeti huwa kati ya trilion 2-2.5 lakini Zanzibar huchangia sifuri katika Mfuko huo wa Muungano uitwao JVC committee. Wakati huo bajeti ya Zanzibar ni kati ya 500b hadi 550b lakini pato la Zanzibar ni 150b, hivyo kiasi cha zaidi ya 350b huwa tunawachangia sisi tani kodi zetu zinakwenda kuwahudumia wao kule... Baada ya hapo katika baje ya Muungano hutengwa 34b kwaajili ya Rais wa Zanzibar, hii huitwa pesa maalumu ikitumika kwa shughuli maalumu za kiusalama na mengineyo... Hii inatoka pia kwa walipa kodi wa Tanganyika, Je Zanzibar inachangia nini kwa Tanganyika? Jibu ni sifuri..... Zaidi ni ulinzi wa Bahari na UDUGU.
Hili ndilo linanifanya nimuunge mkono rais wangu kipenzi...