Mimi ni miongoni mwa watu ninaotatizwa sana na ukiukwaji wa haki unaofanyika popote ndani ya JMT na ni miongoni mwa watu wa mwanzo mwanzo kabisa kumuita rais wetu Dr.John Pombe Magufuli kuwa ni dikiteta.
Katika tumbua tumbua majipu ya rais Magufuli niliunga mkono dhana nzima ya utumbuaji na dhima ya utumbuaji ila sikuunga mkono utekelezaji wa utumbuaji huo kutokana na baadhi ya utumbuaji kufanywa kidikiteta kwa chuki, papara na double standards za hali ya juu kwa kukiuka sheria, taratibu na kanuni.
Lakini kwa hii timua timua ya kuwatimua vigogo wa CCM, nimefarijika sana kwa sababu kumbe huu utumbuaji wa kidikiteta sio kwa serikali tuu bali hata kwa CCM. Hii ni plus kwa Magufuli kuwa katika tumbua tumbua, anatumbua tuu bila kumuangalia mtu usoni kuwa nani ni nani, kama mtu kama Sofia Simba ameweza kutumbuliwa, then kiukweli Magufuli sio mchezo! .
Hakuna ubishi kuwa CCM ni chama kikongwe kinafanya mambo yake kiutu uzima. Kwenye katiba yake kinazo taratibu za nidhamu zilizofuatwa ndani kwa ndani, kimya kimya hadi kufikia hatua ya mwisho ya watu kupigwa chini ndipo umma unaambiwa na kupigwa na surprise. Huu ni ukomavu na ndiko kufanya maamuzi makubwa kiutu uzima. Pongezi ziende kwa Mwenyekiti Magufuli. Wapinzani mjifunze kutoka CCM.
Ugomvi wa Baba na Mama.
Mara nyingi watoto huwa hawawezi kufahamua kuwa kumbe baba na mama huwa wanagombana mara mara ugomvi wa kimya kimya chumbani. Mara kwa mara wanawake huwa wanachukia na kuwanyima 'chakula' waume zao, hivyo kuna wanaume kibao hulala njaa na hawasemi. Kuna wanawake kibao hubakwa na waume zao na wengine hupokea hadi vipigo lakini hawasemi. Kuna mara kibao baba na mama wamenuniana ila akija mgeni warajikausha.
Ugomvi ukiwa mkubwa hadi mama kufungasha ndipo hakuna namna lazima watoto watajua. Hiki ndicho kilichofanyika CCM.
Watuhumiwa wote walijadiliwa toka vikao vya chini kimya kimya. Wakapewa barua za mashitaka yao, wakapewa muda wa kujibu tuhuma, wakaitwa kujieleza, wakahojiwa na kupewa muda wa haki ya kusikilizwa na kujitetea, kisha vikao vikafikia maamuzi kimya kimya na hatimaye ndipo vikao vya maamuzi vikatangaza maamuzi yale. Huu ni ukomavu wa hali ya juu na CCM kinastahili pongezi za dhati kwa hili.
Siku Polepole akiongea na media, awahakikishie Watanzania kuwa taratibu zilifuatwa vinginevyo kama ule udikiteta wa kukanyaga katiba ya nchi pia umeikanyaga katiba ya CCM hivyo timua timua ile ni muendelezo wa udikiteta ule ule, CCM kitakuwa ni chama cha kidikiteta na kama kinaongozwa kidikiteta na kiongozi dikiteta, then jiulize taifa letu la Tanzania tunalipeleka wapi? .
Chedema utumieni uzoefu na ukongwe wa CCM katika kufanya maamuzi yake kwa kuzingatia katiba zenu, niliwahi kuwashauri hivi kuhusu udikiteta katika kuendesha mambo yenu ya ndani.
Fanyeni mambo yenu kimya kimya, jifunzeni kwa CCM ili angalau 2020 Watanzania tuweze kuwafikiria tuwajaribishe vinginevyo tutaendelea kiongozwa na chama kikongwe kilichozeeka mpaka basi lakini kila kinapofanya face lift kama hii, kinarudia ujana hivyo hata hapo mlipo kama mnajidhania mmesimama, angalieni msianguke come 2020.
Hongera sana CCM kwa mabadiliko. Hongera kwa ukomavu.
Jumatatu njema
Wananikera sana CHADEMA siku hizi,nakumbuka enzi za Dk.SLAA.
ReplyDeleteSasa nasikia wanawakaribisha hao waliochwa na FISIEM bila kuwajadili.
Sasa, kama CCM isipotimua-timua watu wake, hiyo Chadema yako itapata wapi wagombea hasa wa uraisi mwaka 2020??
ReplyDelete