Trump apendekeza mchinjo wa hali ya juu kwa misaada ya Afrika

Rais wa Marekani, Donald Trump amependekeza punguzo kubwa la fedha nchi yake inazotoa kwa Umoja wa Mataifa na shirika la misaada la USAid.

Kwenye pendekezo la bajeti hiyo iliyopewa jina, America First: A Budget Blueprint to Make America Great Again, Trump amepanga kuongeza matumizi ya jeshi hadi kufikia dola bilioni 54 kwa kupunguza kiwango katika maeneo mengine.

Amependekeza kuondolewa kwa msaada wwa dola milioni $28.2 kwa African Development Foundation, shirika la Marekani ambalo hutoa ruzuku hadi ya $250,000 kwa jamii na biashara ndogo ndogo katika nchi zilizopo chini ya jangwa la Sahara.

Rasimu hiyo ya bajeti kama ikipita, itaanza kufanya kazi mwezi October, na itaathiri kwa kiasi kikubwa mpango wa chakula duniani (WFP). Kupungua kwa bajeti hiyo kunaamisha kuwa mashirika ya kulinda amani na yale ya shughuli za kibinadamu yatapaswa kupanga upya bajeti zake.

“I propose to reduce funding to the UN and affiliated agencies, including UN peacekeeping and other international organisations, by setting the expectation that these organisations rein in costs and that the funding burden be shared more fairly among members. The amount the US would contribute to the UN budget would be reduced, and we would not contribute more than 25 per cent for UN peacekeeping costs,” maelezo kwenye bajeti hiyo inayopendekezwa yanasema.

Marekani huchangia takriban dola bilioni 10.4 kwa mashirika ya kimataifa ambapo dola bilioni $8.8 huenda kwa Umoja wa Mataifa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad