Kelele nyingi kuhusu Makonda na umaarufu wa jina la Daud Bashite uliopo sasa, umenifanya nione kuwa kumbe Watanzania wakiwa na mshikamano na kuhoji jambo linawezekana.
Kelele za mitandaoni kuhusu Makonda kama zingetumika kuhoji mahali alipo Ben, zingef APATIKANE
Kelele nyingi kuhusu Makonda na umaarufu wa jina la Daud Bashite uliopo sasa, umenifanya nione kuwa kumbe Watanzania wakiwa na mshikamano na kuhoji jambo linawezekana.
Kelele za mitandaoni kuhusu Makonda kama zingetumika kuhoji mahali alipo Ben, zingefanya mamlaka za nchi zijue kuwa suala la Ben lina athari kubwa kijamii na halipaswi kufanyiwa mzaha au kupuuzwa.
Mwezi wa nne sasa Ben hajulikani alipo. Inatakiwa watu wapaze sauti na Serikali itambue kuwa siyo rahisi Watanzania wapotelewe na ndugu yao kisha wanyamaze kama hakijatokea kitu.
Naamini kuwa Serikali ikiamua kulivalia njuga suala la Ben, majibu yatapatikana na itajulikana ni wapi alipotelea. Ben hapaswi kupotea kama Mtanzania wa enzi za ujima. Ben ni kijana wa kisasa, akifuatiliwa zipo alama alizoacha zitatoa majibu.
Niliwahi kuandika kuwa Tanzania siyo Alaska, Marekani, ambako watu mamia hupotea kila mwaka pasipo kujulikana walipokwenda. Tanzania ni Tanzania, mtu akipotea tunajua kuna chanzo. Hicho chanzo ndiyo tukitafute na tukijue.
Hivyo basi, kila Mtanzania anapaswa kuhakikisha anaifanya Tanzania yake inakuwa si rahisi kwa matukio ya hovyo, ama kupoteza watu au watu kujipoteza. Watanzania wanatakiwa kuwa na mshikamano wa kuhoji kuhusu Ben na majibu yenye kutosheleza yatolewe.
Zingatia kuwa kama Ben amepotezwa, waliocheza mchezo huo wataendelea kucheza na wengine, ipo siku watakuja kwako au kwa ndugu yako. Ndiyo maana nimesema Watanzania wanatakiwa kuhoji sana ili kama wapo watu hao, wapate ujumbe kuwa Tanzania siyo rahisi.
Hata kama ni Ben mwenyewe alijipoteza, naye apate ujumbe kuwa Tanzania siyo rahisi. Kwamba huwezi kufanya mchezo wa hovyo kwa nchi yao kisha ukafanikiwa kwa urahisi tu. Tuendelee kuhoji Ben. Tumuombe Mungu amlinde Ben. Kama kuna watu wamecheza mchezo mchafu, basi Mungu atusaidie kuwabaini.
Ndimi Luqman MALOTO
Ni kweli hapa kuna hoja na maana ya kufuatilia suala hili, hivi kweli Mhe, Tundu Lissu mbona amekaa kimya kwa hili wakati yeye ndiye aliyekuwa naye kwenye Press meeting kuwa kijana huyo aliyekuwa msadizi wa Mhe, Mbowe anatumiwa ujmbe wa vitisho kupitia simu yake ya mkononi, halafu kama wiki hivi ikatangazwa kuwa kijana huyo amepotea, nakumbuka hata familia ya kijana huyo hasa baba yake alilalamika kuwa Mbowe alikuwa anapotezea kuhusu kupotea kwa mwanae huyo. Hivi ni kitu gani hicho kwa taifa letu? hivi ni mtu anaweza kupotea hivihivi ndani ya mipaka yetu na ni Mtanzania mwenzetu? je kesho atapotea nani? inawezekana nikawa mimi au wewe, au hata familia yako yote.Nakuwa na wasiwasi mkubwa kwani kuna taarifa za ukweli za familia moja ambayo yeye na mke wake wamepotea hadi leo hii na hakuna kinachoendelea, hawa walikuwa wanasafiri na gari lao binafsi kutoka Dsm kwenda Mkoa wa Njombe ambapo ndiyo kwao, kufika eneo la Makambako muda usio julikana inaonekana walitekwa na watu wasio fahamika na kuondoka nao sehemu isiyojulikana na kuliacha gari lao Makambako ambapo lilionekana na wananchi asubuhi, hadi leo ninavyochangia watu hao hawajaonekana na hakuna tetesi hata angalau kama wameuawa hata miili yao ipatikane. Hali hii inatisha na kuna haja serikali kuliangaliakwa karibu kwani hii ni aina ya uhalifu hatari(organized Crime).
ReplyDeleteHakika ni ukweli usiofichika kwamba siasa chafu ndio zinataka kutuharibu.
ReplyDeleteNinachokiamini Ben yuko hai na pengine viongozi wake wanajua alipo.Iweje mambo mengine chadema wamesimama kidedea lakini jambo la uhai wa mtu hawapigi kelele wala hawaonyeshi nia ya kufatilia tena na sasa wako kimya kabisaaaa kanakwamba halikuwahi kutokea?
Mara nyingi wapinzani ni wapingaji wa kila kitu hata kama kikiwa kizuri, kikiwa kibaya ndio kabisa watalivalia njuga, watalipigia debe, mapovu yatawatoka kwa mambo yasiyo na maana.........wamemtolea macho Makonda wakidhani wanamkomoa, wamesahau yakwao...., endeleeni tu kumshobokea Makonda, yeye bado anasonga mbele, hajafika hapo kwa kura zenu, mumuwacheeeeeee
ReplyDelete