Ukweli Mchungu Kuhusu Anayejiita Mdogo wa Gwajima...!!!!


Amejitokeza mtu mmoja na kufanya press conference kwa jina anajulikana kama Methusela Gwajima , huyu Bwana ni Mwanasheria na ameajiriwa kwenye law firm ya Francis Stolla ambaye anagombea Urais wa TLS .

Huyu Mwanasheria sio mdogo wake na Gwajima wa kuzaliwa , bali ni ndugu katika Ukoo wao huo, naye ni wa KOLOMIJE .

Historia yake ya Kazi inaonyesha kuwa Aliwahi kuwa Katibu msaidizi wa CCM Wilaya ya Singida na katika Wilaya ya Nzega katika cheo hichohicho kwa nyakati tofauti. Kwa sasa ni miongoni mwa wanasheria wa CCM .

CCM wameamua kumtuma kada wao wakifikiri kuwa anaweza kuaminika au kunyamazisha mjadala wa kudai vyeti halisi vya BASHITE ambaye kwa sasa ana stress nyingi sana na amezidiwa kabisa kabisa , baada ya watanzania kuamua kumuunga mkono Rais Magufuli katika zoezi la kuhakiki Vyeti linaloendelea.

Mjadala wa BASHITE utashika kasi sana kwenye vikao vya CCM na hasa kwenye Halimashauri Kuu ambako tayari yule Mbunge wa kule Geita ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa ameomba kuwasilisha hoja mahususi kwenye kikao cha Halimashauri Kuu kuwa Bashite anakichafua Chama , hivyo anataka waazimie kuwa aondolewe na kama halitafanyika basi hoja itawasilishwa Bungeni ili kumwazimia PM ambaye yuko kwenye Mamlaka yao.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bashite anacheti chenye div 0 how comes. Sijawah kuona cheti chenye div 0. Gwajima nawe tunamashaka na elimu yako. Achalia mbali kutumiwa na ccm, je alichokiongea kina mantiki kwa taifa? Yes. Nini kazi ya kanisa kufanya siasa. Nina uhakika mambo anayoyafanya Gwajima kanisani yangefanywa tu na shekh msikitini basi inawezekana angeambiwa anafadhili vikundi vya kigaidi. Iko haja ya kuangalia baadhi ya hayo makanisa. Najua Gwajima ameumia sana kutajwa hivyo anachokifanya Kama revenge watu wa namna hii Hawawezi kuwa wa mungu. Watu wa mungu huwa hawana visasi. Maneno yao mengi ni maombi tu KUWA wanamwachia mungu ahukumu. Sote tunafaham kuwa Gwajima aliwahi mtu mwenye heshma, hekhma, busara, wa kanisa fulani. Matusi Ambayo yalifaa kabisa kupoteza waumini wake wote kanisani. Sembuse makonda. Hivi makonda na kadinali nani maarufu. Kulewa si Lazima unywe kilevi. Sadaka tu za waumini zinatosha kudharau watu. Ushauri wangu, hili ni taifa letu mambo yamsingi ya kitaifa yanapaswa tuyafanye Kama taifa. Makonda kaonyesha ujasiri tumuunge mkono. Vyeti ni makatatasi tu sio u tendaji. Kuna maprof wangapi tunawaona wanashindwa kulisaidia taifa. Na wanavyeti vijaa kabati. Vita hivi ni kubwa na ni ngumu. Wapo wasaliti wanajitokeza.

    ReplyDelete
  2. Haya mwandishi ila kaa ukielewa TZ itajengwa na wenye kuthutubu ambao kwa nchi hii wapo wachache nao ni akina Makonda.Tunajua vita dhidi ya Makonda ni kutaka kuzima moto aliouanza wa madawa ya kulevya kwa kuwa tu wahusika na biashara ya madawa ya kulevya wengi ni viongozi wa hii nchi iwe serikalini,kidini au kwenye sekta binafsi.Gwajima anatakiwa amuogope Mungu,sio aseme kuwa hajawahi kujihusisha na madawa labda aseme ameacha kwa sasa.

    ReplyDelete
  3. Enter your comment...GWajima is à rubbish anachofanya ni kupambana na njeo na mwishowe mkuki wa sumu utaingia Mwln mwake maana hakuna mchungaj mnafk dunian

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad