Lugha ni njia ya mawasiliano, ni chombo kinachotumika katika kuwasilisha ile hali ya kuelimika kwa jamii fulani. Wasomi wengi wa Tanzania wamepata elimu katika mataifa kama China, Russia, France, Germany na zile nchi za Scandinavia. Wengi wa wasomi hawa, mwaka wao wa kwanza ulitumika katika kujifunza lugha ya wenyeji, halafu miaka inayofuata ndipo huanza kusomea fani mbalimbali za kitaaluma.
Wale maprofesa ambao wanafunzi wa kitanzania wanalazimika kujifunza mwaka wa lugha ili waweze kufundishwa nao yale masomo ya fani, mara nyingi hawajui kabisa lugha ya kingereza.
Lakini kwa sababu kujua kingereza sio kuelimika, maprofesa hao wala hawaoni aibu kutokuijua lugha ya kingereza. Wameshaelimika kiasi cha kuigawa elimu yao kwa wanafunzi wa kigeni kutoka Tanzania, bila ya wao kulazimika kuwa watumwa wa lugha ya kingereza.
Kuna wale ambao wanamkejeli rais Magufuli, wakisema kwamba hapandi ndege kwenda Ulaya kwa sababu ya tatizo la lugha ya kingereza, wanasema kuwa anashindwa kuongea na wageni wa kimataifa kwa sababu hajui vizuri kingereza. Huyu anayekejeliwa ni msomi wa ngazi ya PHD, ambaye baadhi ya watu wanamkejeli kwa sababu ya kasumba ya kupenda vituu vya kigeni.
Maprofesa wa mataifa yasiyozungumza lugha ya kingereza, waliowafundisha wasomi wetu ambao ndio "vichwa" vya taifa hili, ni watu walioelimika bila hata ya kulazimika kuwa watumwa wa lugha ya kigeni kwao yaani kingereza.
Sisi tuliotawaliwa tunaona fahari kukifahamu kingereza!. Wakati hatuna maendeleo yoyote ambayo yanahusiana na kingereza, ambayo tunaweza kujivunia kwamba yametokana na sisi.
Tunamkejeli rais wetu tukisema kwamba hayuko vizuri kwenye kingereza, wakati hicho kiswahili chenyewe hatukijui!!. Hicho kiswahili ambacho ni lugha ya taifa kinaishia kutamkwa midomoni peke yake, hakuna maendeleo yoyote yale ya kiteknolojia ambayo yanahusishwa na lugha ya kiswahili kwa asilimia mia moja.
Miaka ya nyuma huko migodini wazungu ambao huko Uingereza na Australia walikuwa ni wafungwa, walipewa kazi na kulipwa mishahara mikubwa kwa sababu tu ya kuongea kwao lugha ya kingereza!.
Hawakuwa na utaalamu kuwazidi wataalamu wazalendo waliosomea VETA na vyuo vingine vya ufundi hapa hapa Tanzania. Ulimbukeni wetu ukawapa maisha bora wageni, kwa sababu akili zetu zilinasa kwenye mtego wa kubabaikia kingereza.
Watanzania tuachane na huu ushamba wa kuiona lugha ya kingereza kama vile ndio kila kitu maishani.
ninachofaham kuanzia primary hadi phd kasoma kwa kingereza, sasa inakuwaje anashindwa kuzungumza me sijui.
ReplyDeletepia kama siku ataamua kuzungumza kingereza bas tutabana bajeti ya kumlipa mkalimani kufuatana na raisi