Vita ya Makonda na Gwajima Yafika Lavel Hii..!!!!


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ametaja makosa ya kisheria yaliyomfanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda kukimbilia Afrika Kusini.

Akizungumza jana kanisani kwake, Ubungo, jijini hapa, Gwajima alidai  kosa la kwanza la Makonda ni kughushi cheti ambacho kinaonyesha yeye ni Paul Makonda wakati akifahamu kuwa yeye ni Daudi Bashite.

“Kosa hilo kwa mujibu wa Gwajima ni kifungo cha miaka saba.Kosa jingine ni kula kiapo cha ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa akisema yeye ni Makonda wakati akijua yeye ni Bashite,” alisema

Gwajima alisema  kosa la hilo la kula kiapo na cheti feki  ni kifungo cha miaka mitatu.

Kosa jingine  alisema ni kupokea mshahara na posho kwa jina la Makonda wakati akifahamu si yeye   na kuongeza kuwa kosa hilo likithibitika atatakiwa kurudisha mishahara na posho zote alizochukua.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. PUMBA TU.KANISA LAKO NI KUHUBIRI SIASA?AU INJILI?

    ReplyDelete
  2. Gwajima mbona hukusema yote hayo kabila hujashikwa, bada ya kushikwa unalipiza kisasi. Ugekuwa unataka kusema ukweli ugesema kabla hujashikwa hii ni kulipiza lisasi tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad