Walimu Wakuu wa Shule Zilizofanya Vibaya Darasa la Saba Wakabidhiwa Vinyago Vyao...!!!


Walimu wakuu wa shule za msingi Magunga na Lubanta, Wilaya ya Mvomero zilizofanya vibaya kwenye mtihani wa darasa la saba mwaka jana, wamekabidhiwa kinyago.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utaly alikabidhi kinyago hicho katika tukio lililoshuhudiwa na walimu wakuu wa shule za msingi na waratibu elimu kata wa wilaya hiyo, shule hizo zitakaa na kinyago hicho kwa kupokezana ndani ya miezi sita kila shule.

Shule zilizofanya vizuri zimepatiwa vyeti maalumu vilivyosainiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ili ziongeza bidii.

Ofisa Elimu ya Msingi wilayani Mvomero, Michael Ligola alisema kutokana na wilaya hiyo kufanya vibaya kitaaluma katika matokeo ya mwaka jana, walifanya utafiti mdogo wa kuzunguka kwa baadhi ya kata kuona kilichosababisha hali hiyo.

Ligola alisema asilimia 80 ya matatizo waliyoyabaini katika maeneo mengi uwezo wake upo ndani ya maeneo husika, ikiwamo kuwahusisha wakuu wa shule na waratibu.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. duh kinatishaa ahaaa kweli huwezi kutamani kua nacho

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad