Wapenzi Watiwa Mbaroni kwa Kufanya Mapenzi Kabla ya Ndoa...!!!!


RAIA mmoja wa Afrika Kusini na mchumba wake kutoka nchini Ukraine wametiwa mbaroni nchini Falme za Kiarabu kwa kufanya mapenzi kabla ya ndoa, ndugu amebainisha.

Emlyn Culverwell, 29, na Iryna Nohai, 27, waliripotiwa kukamatwa baada ya daktari kugundua kwamba Nohai, ambaye alikuwa na maumivu ya tumbo, alikuwa na ujauzito.

Walikamatwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa, jambo ambalo ni kinyume cha sheria nchini humo.

Mama wa Culverwell ameomba waachiwe huru, kwa kusema “kitu pekee walichofanya kibaya ni kupendana.”

Wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini ilisema kwamba haitoweza kuwasaidia wapenzi hao kwa kuwa ni suala la ndani la sheria za Falme za Kiarabu, mtandao wa News24 uliripoti.

Serikali ya Afrika Kusini imewashauri wapenzi hao kutafuta msaada wa kisehria, mwandishi wa BBC huko Johannesburg anasema.

Hadi sasa hakuna maelezo yoyote kutoka serikali ya Falme za Kiarabu.

Culverwell na Nohai wanaripotiwa kuwa wanashikiliwa tangu mwezi Januari mwaka huu, lakini taarifa juu ya kushikiliwa kwao zimeanza kujulikana sasa.

Culverwell amekuwa anafanya kazi nchini Falme za Kiarabu kwa miaka mitano sasa.

Mama yake Linda aliuambia mtandao wa News24 kwamba familia yake inajaribu “kupeleka ujumbe kwa wawili hao na kuwaambia kuwa inawapenda na kwamba hawapaswi kuwa na wasiwasi.”

Wapenzi hao bado hawajafunguliwa mashtaka kwa kuwa mamlaka nchini humo bado wanawafanyia uchunguzi wa kiafya.

Iwapo watakutwa na hatia, wanaweza kukabiliwa na kifungo cha muda mrefu.

FacebookTwitterGoogle+WhatsAppPinterestShare

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad