Wema Afanya Jambo Siku ya Wanawake Duniani..!!!


Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu ameshiriki kwa kupanda miti katika vyanzo vya maji vya Mbogo na Nukutu katika milima ya Uluguru, Manispaa ya Morogoro.

Wema aliyeungana na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Morogoro kupitia CHADEMA, Devotha Minja, Diwani wa kata hiyo pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa, wamefikia hatua hiyo kwa lengo la kuhifadhi vyanzo vya maji ambavyo vimekuwa vikiharibiwa kwa kiasi kikubwa katika maeneo hayo, hali inayotishia maisha ya viumbe pamoja na wakazi wanaotegemea vyanzo hivyo.

Mrembo huyo ambaye pia msanii wa filamu nchini, amesema kuwa ameamua kuunga mkono jitihada hizo za kuhifadhi vyanzo vya maji ili kuondoa kero za maji ambazo wanawake hukumbana nazo, huku akitoa somo kuwa faida na manufaa ya miti hiyo zitaonekana baadaye.

"Leo ni siku ya wanawake duniani, nikaonelea nijiunge na wanawake wenzangu wa Mkoa wa Morogoro siku ya leo katika upandaji wa miti ambao utakuja kuwa na tija kwetu na kupunguza kero kubwa inayotukabiri ya maji, wote tunajua kuwa mwanamke ndiyo anakerwa zaidi katika upatikanaji wa maji labda haittusaidia leo wala kesho lakini itakuja kusaidia vizazi vyetu vya baadae". Amesem Wema Sepetu.

Wema ambaye hivi karibuni ametangaza kujiunga na CHADEMA akitokea CCM, amesema ameongeza kuwa mazingira hayana itikadi wala vyama na kwamba yanamgusa kila mtu hivyo yampasa kila mmoja kupanda miti ili kuweza kulinda vyanzo vya maji.

Kwa upande wake Mbunge Devotha Minja ambaye kabla ya kuwa mbunge amekuwa akiripoti habari nyingi kuhusiana na uharibifu wa mazingira kupitia kazi yake ya uandishi wa habari, amesema ameamua kuchukua hatua kwa vitendo kama kiongozi ili kuwa mfano kwa jamii nzima ya watanzania hususani wakazi wa Morogoro, kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad