Yafahamu Makundi Manne ya Binadamu...!!!


Binadamu kama walivyo viumbe wengine, hutofautiana kwa mambo mengi. Kwa kushindwa kutambua tofauti zilizopo baina yao, binadamu wamekuwa ni viumbe wanaoongoza kwa migogoro. Kwa kuzingatia hilo, nimekuandalia mada inayohusu aina na makundi ya binadamu. Naamini baada ya kufahamu tabia na hulka tofauti za binadamu, migogoro isiyo ya lazima itaepukwa.

Binadamu wanagawanywa katika makundi makuu mawili kulingana na uwezo wao wa kufikiri na kuchanganua mambo.Makundi hayo mawili yamegawanyika mara mbili na kutengeneza makundi makuu manne kama ifuatavyo:​

1.Introvert- Hili ni kundi linalojumuisha binadamu wenye uwezo mkubwa kiakili na wanaotafakari mambo kwa kina, Binadamu wanaopatikana katikakundi hili hutofautiana kwa kiasi kikubwa na wengine kutokana na uwezo wao wa akili (Intelligent Quotient). Kundi hili nalo limegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni:

A. Melancholy: Binadamu katika kundi hili ni wenye upeo mkubwa wa kuvumbua mambo ya kitaalam yanayohitaji akili nyingi na wana uelewa mpana kwenye masomo ya Sayansi na Hesabu. Licha ya uimara huo katika akili zao, binadamu wa kundi hili wana hisia zinazogusika na kuchokozeka kirahisi. 

Wanawake ni wepesi wa kulia pale wanapokerwa hata na jambo dogo, Wana upendo wa dhati lakini wanapotendwa hata kwa jambo dogo, huumia sana kihisia. Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa. Wana aibu sana wawapo mbele ya watu wengi na ni watunzaji wazuri wa siri.

B. Phlegmatic:
Hili ni kundi la binadamu ambao wana uelewa mpana, wana uwezo wa kuchanganua mambo kwa kina na kujenga hoja lakini hawawazidi binadamu wa kundi la kwanza (Melancholic). Wana hisia ngumu, siyo waoga na wanajijali wao kuliko watu wengine.

Ni wabishi na hupenda kutumia mifano na takwimu katika ubishi wao. Hawayapi mapenzi kipaumbele katika maisha yao nawengi huishi single' kwa muda mrefu. Wanajiamini sana hata kwa mambo ambayo hawayajui.Wengi hupenda kuchunguza na kufuatilia maisha ya wengine na wanafaa kwa kazi za ushushushu.

2. Extrovert: Hili ni kundi kuu la pili linaloundwa na binadamu wenye uwezo wa kawaida wa kiakili. Uwezo wao wa kuchanganua mambo ni wa kawaida, hawajishughulishi kujua mambo yasiyo na manufaa na ni wepesi wa kuridhika hata kwa mafanikio madogo. Kundi hili nalo limegawanyika katika makundi makuu mawili:

A. Sanguine- Kundi hili linaundwa na binadamu wenye uwezo wa kawaida wa kiakili, kufikiri na kuchanganua mambo (wakati mwingine huwa na uelewa mdogo). Ni wacheshi, wanapenda sifa, wanapenda kusikilizwa kuliko kuwasikiliza wenzao na hupenda kuwa wazungumzaji wakuu kwenye kila jambo hata kama hawana ufahamu nalo. Ni wagumu wa kutunza siri.

Hawapendi kujifunza mambo mapya na hata wakifundishwa husahau haraka. Wanapenda sana kuonekana kwa watu kwa kila jambo wanalolifanya hata kama ni dogo. Si waaminifu katika mapenzi na siyo ajabu kuwakuta wakiwa na wapenzi wengi kwa wakati mmoja.

B. Choleric- Kundi hili linaundwa na binadamu wenye sifa zinazokinzana na kundi la Melancholic. Wana uelewa mdogo katika kila jambo na wengi hukatisha masomo yao kutokana kuwa na vichwa vizito. Ni wakali, wakatili na wana wivu kwa mafanikio ya watu wengine

Tabia ya kila kundi, tunaendelea na uchambuzi wetu kwa kutazama tofauti kati ya kundi la Introvert na Extrovert.

Tofauti zote zinaanzia kwenye asili ya kila kundi. Kundi la kwanza (Intovert), asili yake ni kusikiliza na kuufuata msukumo wa nguvu kutoka ndani bila kutegemea mazingira ya nje wakati kundi la pili (Extrovert) husikiliza na kufuata msukumo wa nje ya miili yao. Hisia zao hutegemea mazingira ya nje kuliko ya ndani.

1: Ukimya
Binadamu wanaopatikana katika kundi kuu la kwanza, Introvert ni wakimya sana, wanaona aibu kuzungumza mbele ya binadamu wengi ingawa wanapenda kufanya mambo kwa vitendo. Wanaelewa zaidi kwa vitendo nahawaamini kwa urahisi kile wanachokisikia bila kuona vitendo.

Binadamu wanaopatikana katikakundi la pili ni kinyume chake. Extrovert wanapenda sana kuzungumza na kubishana mbeleya wengine hata kama hawana uhakika juu ya kile wanachokibishia. Ni wepesi wa kuamini maneno ya wengine bilakutafakari kwa kina na hupotoshwa kirahisi. Ni wagumu wa kuonesha vitendo juu ya yale wanayoyasema.

2: Uvumilivu
Binadamu wanaopatikana katika kundi la kwanza, Introvert ni wavumilivu katika mipango ya muda mrefu na hawaoni hasara kulifuatilia jambo moja hata kwa kipindi kirefu. Hawajali linaumiza kichwa kwa kiasi gani ilimradi wafanikiwe. Mara nyingi wanapenda kufanya kazi peke yao na kuwaonesha wengine matokeo.

Kundi la pili ni kinyume chake. Extrovert wanapenda sana kazi nyepesi nyepesi zisizoumiza kichwa na zinazokamilika haraka.Hawapendi kazi ngumu zinazochukua muda mrefu kukamilika na hulka hii inawaweka mbali na mafanikio ya muda mrefu. Wanapenda kufanya mambo katika jumuiya kuficha udhaifu wao na wanapofanikiwa hata kwa kiasi kidogo, hujisifu sana.

3: Marafiki
Kundi la kwanza la binadamu (Introvert) huwa na idadi ndogo ya marafiki kutokana na haiba ya ukimya na kuona haya kuzungumza na wengine kwa mambo ambayo wanayaona siyo ya manufaa. Wengi ni wakimya na hawawasiliani sana na wengine kutokana na asili yao, hali inayowafanya wawe na marafiki wachache. Hata hivyo, marafiki wanaokuwa naohudumu nao kwa kipindi kirefu. Kundi la pili ni tofauti kwa sababu ya haiba yao ya uzungumzaji na ucheshi hupata marafiki wengi na kufahamika kwa urahisi kutokana na kupenda kuonekana kwa wengine lakini mara nyingi marafiki wanaokuwa nao hudumu nao kwa kipindi kifupi.

4: Mavazi
Kundi la kwanza (Introvert) hupendelea mavazi ya kawaida yanayowafanya wawe huru kufanya mambo yao. Hawapendikujipamba sana kwa vito au nakshi nyingi, wanapenda kuonekana simple lakini nadhifu. Wanavutiwa na rangi zilizopoa. Kundi la pili ni tofauti. Extrovert wanapenda sana mavazi yanayowafanya waonekane wanazo', hupenda kujiremba kwa mavazi ya bei ghali, vito na vidani vingi kwenye miili yao (hasa wanawake). Wanapenda sana rangi zinazong'aa na kuonekana kwa urahisi. Hii ni kwa sababu popote walipo wanataka wengine wawaone. Huwa hawajali unadhifu bali hupendelea mavazi na vitu vya bei ghali.

Tofauti ya tano na ya mwisho inayohusu uhusiano wa kimapenzi.

5. MAPENZI
Kama tulivyoona katika matoleo yaliyopita, binadamu wa kundi la Extrovert wanaongozwa na nguvu za msukumo na hisia kutoka nje (mazingira wanayoishi). Tuliona kwamba binadamu wanaopatikana katikakundi hili ni waongeaji sana, wacheshi, wanaopenda kuonekana na sifa nyinginezo nyingi.
Tuliona pia kuwa binadamu wanaopatikana katika kundi la Introvert wana sifa zinazokinzana na wale wa kundi la kwanza. Ukimya, kupenda kusikiliza kuliko kuzungumza, ugumu wa kuwasiliana na wengine na kuongozwa na hisia na msukumo kutoka ndani ni baadhi ya sifa zinazowafanya binadamu wa kundi hili wawe tofauti na wengine. Inapotokea binadamu wa kundi la kwanza akawa na uhusiano wa kimapenzi na mwingine kutoka kundi la pili, je, uhusiano wao utadumu? Hili ni swali la msingi tunalopaswa kujiuliza. Migogoro mingi ndani ya ndoa na uhusiano wa kimapenzi husababishwa na wahusika kushindwa kuelewa tofauti zilizopo kati yao na wanaowapenda. Ni makosa kulazimisha mwenzako afanane na wewe bila kuzingatia tofauti za msingi zilizopo baina yenu. Hii ndiyo sababu ya msingi ya kumchunguza na kumwelewa mwenzi wako kabla hamjaingia katika maisha ya ndoa kwani ukishindwa kumuelewa mwenzako utaangukia pua.

Soma mfano ufuatao: Salum na Miriam ni wapenzi waliokaa pamoja kwa miezi kadhaa. Tabia na mwenendo wa Salum unamfanya Miriam ahisi kwamba hapendwi ila analazimisha kupendwa (anajipendekeza). Siku zote malalamiko yake ni kuwa Salum hamjali, hapendi kuzungumza naye mpaka alazimishwe na ni mgumu sana wa kutoa siri zake, hali inayomfanya Miriam ahisi kuwa huenda ana mpenzi mwingine anayempenda zaidi yake.

"Mimi ni mcheshi sana, napenda kufurahi na kupiga stori na marafiki. Nafahamika na kuheshimika na wengi lakini mpenzi wangu yuko tofauti. Ni mkimya sana, anapoongea na mimi haniangalii usoni na mara zote yeye huwa msikilizaji tu bilakuchangia chochote katika hoja ninazozianzisha. Hana marafiki wengi na hupenda kujitenga kuliko kukaa na mimi," analalamika Miriam.

Tatizo hapa linasababishwa na utofauti wa asili uliopo kati ya Salum na Miriam. Salum anapatikana katika kundi la pili labinadamu (Introvert) na Miriam anapatikana katika kundi la kwanza (Extrovert). Kwa kushindwa kufahamu tofauti iliyopo kati yake na mpenzi wake, Miriam anahisi Salum hampendi. Laiti kama angejua kuwa kuna tofauti kubwa kati yao, angejua namna ya kukabiliana na hali hiyo.

Matatizo kama hayo huwakumba wengi, Cha msingi hapa ni kufahamu tofauti zilizopo na kuwa tayari kuendelea kujifunza. Introvents wana asili ya ukimya na ni wagumu wa kuwasiliana na wengine lakini hiyo haina maanakwamba hawayawezi mapenzi. Ukiweza kufahamu tofauti na kuzichukulia kama changamoto, watu wa kundi hili jhuwa na upendo wa dhati kuliko Extrovert. Wakianzisha uhusiano huwa wanataka udumu kwa kipindi kirefu zaidi.

Karibuni kwa mjadala zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad