Leo Ijumaa February 3, 2017 uongozi wa Yanga umesitisha mkataba na mkurugenzi wao wa ufundi Hans van Pluijm.
Van Pluijm alikuwa kocha wa timu hiyo kabla ya kubadilishiwa majukumu kuwa mkurugenzi wa ufundi baada ya ujio wa George Lwandamina ambaye ndio kocha mkuu wa sasa.
Taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zinataja kuwa chanzo cha kuondoshwa kwa kocha huyo ni uhaba wa pesa unaoikabili klabu hiyo kwa sasa.
Udaku Blog inaendelea kupambana kutafuta sababu zilizopelekea Pluijm kupigwa chini na Yanga na habari kamili utaipata hapahapa.