Zaidi ya Watu 30 Wanahofiwa Kuuawa Afghanstan


Zaidi ya watu 30 wameuawa, kulinga na maafisa, lakini baadhi ya ripoti zinasema kuwa idadi ya vifo huenda ikawa kubwa zaidi.

Makamanda wa Afghanstan tayari wametua kwenye paa la hospitali hiyo ya Sardar Daud na sasa wanapigana na wanamgambo.

Kundi la Islamic State(IS) limedai kuhisika na shambulio hilo.

Taleban wamekanusha kuhusika, kulingana na ripoti ya vyombo nchini humo.

Rais Ashraf Ghani amesema kuwa shambulio hilo kwenye hospitali ya Sardar Daud hospital yenye uwezo wa kuwalaza wagonjwa 400 ni "uvunjaji wa maadili yote ya binadamu".

" Katika dini zote, hospitali inachukuliwa kama mahala penye kinga na kuishambulia ni kuishambulia Afghanstan nzima ," alisema .

IS wamekuwa wakiendesha harakati zao nchini Afghanistan tangu mwaka 2015 na tayari wamekwisha tekeleza mashambulio kadhaa nchini humo.

Ilidai kuwajibika na ulipuaji wa mashambulio ya kujitoa muhanga katika mahakama kuu ya mjini Kabul mwezi uliopita ambapo watu 22 waliuawa.

Kundi linalojiita jimbo la Khorasan, ambalo linaunganisha mataifa ya Afghanistan na Pakistan, hivi karibuni limeanza harakati zake katika mataifa yote mawili.

Wapiganaji wa Taleban pia wamekuwa wakiendesha mashambulio yaliyowauwa watu 16 mjini Kabul katika mashambulio yaliyokuwa ya kujitolea muhanga.

Shambulio lilianza saa tatu unusu kwa saa za Aghanstan wakati mwanamgambo alipojilipua katika lango moja la upande wa kusini mwa hospitali- ambayo iko karibu na ubalozi wa Marekani- halafu washambuliaji wengine watatu wa wakaingia ndani ya mazingira ya hospitali hiyo.

Wakaingia katika ghorofa la pili na la tatu huku wakiwa na silaha ndogo pamoja na gurunati na kuanza kufyatua risasi.

Mhudumu mmoja wa hospitali ambaye aliweza kutoka nje alimuona mshambuliaji "akiwa amevalia koti jeupe amesikilia bunduki aina ya Kalashnikov na kumfyatulia risasi yeyote, wakiwemo walinzi, wagonjwa na madaktari". Mhudumu mmoja aliandika kwenye ukurasa wa Facebook: "washambuliaji wako ndaniya hospitali. Tuombeeni."

Mmoja wa washambuliaji ameuawa na wengine walikuwa wamejificha chini ya ngazi, alisema msemaji wa wizara ya ulinzi. Askari mmoja pia ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa na wagonjwa wanaokolewa kupitia milango ya kutokea ya dharura.

Takriban watu watatu wamekufa na wengine zaidi 60 wamejeruhiwa, wengi wao wakiwa ni wahudumu wa hospitali, amesema waziri wa afya na pia vyombo vya habari.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad