Alichokifanya Rais Wakati wa Kumsindikiza PM wa Ethiopia ni "Aibu" Kiitifaki,Wahusika Msaidieni..!!!


Kwanza tunapaswa kujua vile vikundi vya ngoma na utamaduni wakati wa kupokea ugeni wa nchi au kusindikiza/kuaga huwa wanalipwa,na kazi ya kuvikusanya na kuvipeleka Airport ipo chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dsm.

Wale Wamama unaowaona wanapepea bendera za nchi mwenyeji na nchi mgeni huwa ni Walimu wanaochukuliwa katika shule za mkoa wa Dsm.Wengi ni walimu wa Shule ya Msingi.

Awali malipo yao ilikuwa ni shilingi 20,000 ila kwa sasa wamepandishiwa mpaka shilingi 50,000 kwa siku.Hivyo bajeti yao huwa ipo.Na vile vikundi vya ngoma huwa ni kutoka JKT au JWTZ.Wale wote wana posho yao.

Jana kama mlivyomsikia Rais,anasema ameamua kuwapa hiyo zawadi ya milioni 20 sbb wameonyesha uzalendo na ukarimu kwa wageni na kuiletea nchi sifa,lakini Rais akasema anajua huko nje wanasemwa sana na kuchekwa kuwa wanapoteza muda,hivyo kuwatia motisha akatoa milioni 15 na Waziri Mkuu Milioni 5.

Jambo la Kujifunza::

1)Kwanza nafikiri huu utaratibu wa Rais kumwaga mwaga pesa si jambo la ajabu sana,lkn linapaswa kuratibiwa vizuri,yaani washauri wake wampe kamuongozo tu ka namna ya kuzifikisha na kuwatia moyo anaokusudia kuwapa motisha.Hizi hela za hivi kwa JK zimeliwa sana,lkn hazikuwa na "Promo" kama hii.Nafikiri Rais anatumia utaratibu wa kutangaza na watu kugawiwa papo kwa papo sbb enzi za JK ikitolewa milion20 wale wamama wanakutana na milion10.Hizi kumi zinapotelea hapa katikati kutoka benk mpaka kwa kina Mama "upepo" unaziyeyusha hizo 10

2)Haka ka utaratibu ka kumstukiza mtu achangie papo kwa papo sio kazuri,maana ukiangalia hiyo ya Airport,Rais kachukua kipaza kaahidi milioni 15 hapo hapo akampasia Majaliwa naye aahidi,mpaka Majaliwa akapata kigugumizi akasema "Nilidhani protocol hazikubali,lakini kama mkubwa kasema,basi mi sitatoa nyingi kumzidi,mi ntawapa milioni 5".Hii ilitokea hata kule Nangurukuru,Rais anatoa milioni 20 ya Zahanati halafu anampa DED atoe milioni 10 na Mbunge anaambiwa atoe,aliposema hana akamnanga.

3)Jana Rais amevunja Protocol,kwenye itifaki ya "Arrival and Departure Protocol of State Visit at Airport" kuna mambo ya kuzingatiwa.

Wakati wa "Arrival",ni kawaida uwanja kufungwa nusu saa kabla ya mgeni kutua na kusubiri ametua na kupokelewa.Then Chief of Protocol akiwa na balozi wa nchi ya mgeni wanapanda kwenye ngazi kwenda kumpokea mgeni,anashuka,anapewa maua na mtoto aliyeandaliwa na baadae anasalimiana na mwenyeji,huku akimtambulisha kwa viongozi kwa itifaki. ile "Guard of Honour" inaweza kuwa "Silent" au ile ya mizinga 21.

Wakati wa "Departure" kadhalika uwanja hufungwa,hivyo ndege nyingine huendelea kuzunguka juu mpaka shughuli za kumuaga na ndege kunyanyuka zikamilike,na zile zilizo chini,husubiri mpaka ndege ya mgeni mashahuri iondoke.

Wakati wa kuondoka kwanza hupigwa nyimbo za nchi zote,then anasindikizwa mpaka kwenye mlango wa ndege...anaagana na na wenyeji na baadae anapanda peke yake hadi katika ngazi ya mwisho,anageuka na kupunga mkono na kuingia ndani.Na ujumbe uliombatana nae hufuata kuelekea ktk ndege kwa haraka tyari kwa safari.

Rais au msindikizaji (anaweza kuwa Waziri wa Mashauriano ya kigeni au yoyote) huendelea kusimama pembeni mpaka pale mgeni wake ktk ndege itakaponyanyuka "take off" kutoka kwenye runway,na ndipo bendera ya rais mgeni inashushwa kuashiria kuwa hayupo tena katika eneo lile kama mgeni.Hii ni heshima kwa mgeni na wawakilishi wake kama balozi waliobaki nchini na kwa nchi ya Rais mgeni.

Lakini jana sijui watu wa Protocol ilikuwaje,walipaswa kumwambia mkuu asubiri ile ndege ya Waziri Mkuu inyanyuke kutoka katika ardhi ya nchi yake na bendera ya Rais wa Ethiopia kushushwa ndio aende kwenye wale wanavikundi wa ngoma na utamaduni.Sasa kwenda wakati ndio kwanza ndege inaelekea eneo la kurukia ni "mapungufu madogo ya itifaki" ambayo yanapunguza "uweledi" wa wanadiplomasia wetu katika medani za kimataifa.Ni kukosa "heshima" za kiitifaki kwa mgeni na ujumbe wake,ni kuleta picha mbaya kwa balozi wa Ethiopia Tanzania aliyekuwa uwanjani kuambatana na Rais kumsindikiza Waziri Mkuu wake.

Hii si picha nzuri,siku zijazo viongozi wetu wanaweza tumika kama "rejea" (references) ya mfano wa viongozi wanaoongoza kuvunja taratibu za kiitifaki na tukabaki katika kumbukumbu zisizo nzuri katika medani ya kimataifa.Haya yalitokea kwa Amini miaka ile ya utawala wake.Kumbe si ajabu nchi nyingi duniani huwaandaa viongozi wakuu wa nchi na serikali kwa kuwaweka katika wizara ya mashauriano ya kigeni kwa muda kabla kama njia ya kuwaandaa kuwa viongozi wakuu.

Ndio maana wakati PM Majaliwa kapewa kipaza atoe ahadi kwa wale kina Mama alisema "Mimi mwenyewe nilivutiwa na jinsi mlivyocheza na kuimba,lakini nilidhani mambo ya protocol hayaruhusu kuja hapa,siwezi kuahidi kiasi kikubwa zaidi ya mkubwa wangu,mimi nitatoa milioni 5"

Tutaendelea kumkumbusha Rais wetu sababu bado tunampenda.Sisi tuliompigia kampeni na kumpa kura tutaendelea kusema ili kumfanya awe bora zaidi na zaidi.Ukosoaji wetu usichukuliwa kama nia mbaya kwa Raisi,bali upendo wa kweli wa kumfanya awe bora zaidi na zaidi.Maana siyekupenda hakuthamini.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuna watu hatawaki Rais akosolewe hata ktk mambo ya msingi yayoweza kutia nchi yetu aibu.jambo ni jemaK,lilipaaswa kufanyika baada ya ugeni kuondoka.Kwa mambo km haya Mkuu anapaswa kusikiliza ushauri

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad