Alichokisema Rais Magufuli Baada ya Askari Nane Kuuawa Mkoani Pwani..!!!


Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari Polisi 8 waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha jana jioni katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.

Askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na wameshambuliwa kwa kupigwa risasi wakiwa wanasafiri kwa gari katika barabara ya Dar es Salaam – Lindi.

Mhe. Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP-Ernest Mangu, familia za askari wote waliouawa, Askari Polisi wote na Watanzania wote walioguswa na vifo hivyo. 

“Nimeshtushwa na nimesikitishwa sana na vifo vya askari wetu 8 ambao  wamepoteza maisha wakiwa wanalitumikia Taifa, naungana na familia za marehemu wote, Jeshi la Polisi na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na vijana wetu shupavu. 

“Namuomba Mwenyezi Mungu atupe moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amelaani tukio hilo na matukio yote ya kuwashambulia askari polisi ambao wanafanya kazi kubwa na muhimu ya kulinda raia na mali na ametaka Watanzania wote watoe ushirikiano katika kukomesha vitendo hivyo.

Mhe. Rais Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wee Ali mpinge tumia busara usiongee mambo ya kijinga.

    ReplyDelete
  2. Ningeomba kwa kutumia iteljensi ya kimtandao ya vyombo vya serikali kumfuatilia na kumchukulia hatua za kisheria huyo mtoa maoni hapo juu anaejiita Ally kwa kushabikia mauaji ya polisi. Na kama yupo nje ya nchi ni vizuri zaidi kuchukuliwa hatua kwa sababu wenzetu huku nje hawana msalie mtume kwa wauaji wa polisi. Vyombo husika wamtafute kutokana na maelezo yake ni miongini mwa wenye mtandao wa kuwa polisi.

    ReplyDelete
  3. Ali Mpinge hata kwenye mwanga anaona giza.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad