Msemaji huyo amedai hajasikizwa kabla ya kutolewa kwa hukumu huku akidai kuwa baada ya kupewa barua iliyomtaka kufika mbele ya kamati ya nidhamu uongozi wa Simba ulitoa taarifa ya udhuru kwamba Manara hatofika mbele ya kamati siku ya Jumapili April 23, 2017 kwa sababu atakuwa nje ya Dar na kuomba kamati ipange siku nyingine ya kusikiza shauri hilo.
“Unazuia na kutonipa nafasi ya kusikilizwa, unanipa hukumu kwa makosa nisioandikiwakatika mashtaka yao, nipo tayari kwa ajili ya mapambano, tukutane juu.” aliandika Manara Instagram.
Kamati ya nidhamu imetoa fursa kwa Manara kukata rufaa kwenda ngazi za juu ikiwa hajaridhika na maamuzi yaliyotolewa.
TFF ilimfungulia mashtaka ya kinidhamu yenye makosa matatu kwenye kamati ya maadili. Kosa la kwanza ni kuongea maneno ya kashfa kwa viongozi wa TFF, kosa la pili kuchochea ukabila na kosa la tatu ni kukosoa maamuzi ya TFF kupeleka suala la Mohammed Fakhi kwenye kamati ya Katiba, Sheria na hadhi za wachezaji.