Aliyezaa na Young D Amfungukia Amber Lulu


BAADA ya picha za msanii wa Bongo Fleva, David Genz ‘Young D’ na Amber Lulu wakiwa kimahaba kusambaa mitandaoni huku habari zikieleza kuwa wawili hao wanapika na kupakua, aliyezaa na mwanamuziki huyo, Mamisa Amir, amefunguka kuwa haoni jipya.

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Mamisa alisema picha na habari za baba mtoto wake huyo, anaona ni jambo la kawaida, kwani asipojiheshimu mwenyewe hakuna atakayemheshimu.

“Hizo habari na picha naona kawaida tu maana mtu asipojiheshimu mwenyewe hakuna atakayemheshimu, niko kwa kina Young D tunalea tu mtoto lakini uhusiano wa kimapenzi ulishaisha,” alisema.

Alipotafutwa Amber Lulu kujibu inakuwaje anajiachia kimahaba na msanii huyo angali akijua ana mtoto na mwanamke mwingine, alisikiliza kabla ya kucheka na kukata simu huku ile ya Young D ikiita bila kupokelewa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad