ARV Zaanza Kuzalishwa Arusha..!!!!


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV), zitaanza kuzalishwa mkoani Arusha na Kiwanda cha TPI ARV Limited ambacho tayari kimepewa leseni.

Ummy alisema hayo jana bungeni alipojibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Fatma Toufiq, aliyetaka kujua iwapo Serikali mpango wowote wa kuanzisha kiwanda cha kutengeneza ARV.

Pia, alihoji iwapo dawa hizo zinazoagizwa na kutumiwa nchini kama zipo na zile zilizotengenezwa maalumu kwa ajili ya watoto.

Waziri Mwalimu alisema kwa sasa kuna kiwanda mkoani Arusha (TPI ARV Limited) ambacho kimepewa leseni ya kutengeneza ARV, ili kufubaza makali ya ugonjwa huo.

Kuhusu dawa zinazoingizwa nchini, alisema; “zipo za watoto ‘Nevirapine Syrup, Lopinavir/Ritonavir Syrup’.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad